Header Ads Widget

MAHAFALI KIDATO CHA SITA SHULE ZA KAIZIREGE NA KEMEBOS YAFANA ,MATUMIZI NA ELIMU YA FEDHA YATOLEWA





Shule za Kaizirege na Kemebos zilizopo katika kijiji na Kata ya Ijuganyondo katika Halmashauri ya  Bukoba  Mkoani Kagera zimefanya Mahafali ya pamoja kwa ajili ya kuwaaga Wahitimu kidato cha sita Mwaka 2024.anaripoti mwandishi wa Matukio Daima App Shemsa Mussa kutoka Kagera 

Mahafali  hayo yaliyohudhuliwa na watu Mbalimbali akiwezo Wazazi,Wanafunzi,Walimu pamoja na Wageni waalikwa  huku Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo akiwa  Bi Ruth Zaipuna Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Bank ya NMB Tanzania. 


Awali akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi  Mwalimu Mkuu wa Shule hizo ,Mwl Kisha Ilamulira amesema Shule ya Kaizirege  ilianzishwa Mwaka 2007 chini ya Mkurugenzi Bw Yusto Kaizirege Ntagalinda na baadae kuanzisha shule nyingine ya Kemebos  na shule zote mbili ni kuanzia awali hadi kidato cha sita na kusema kuwa mpaka sasa wahitimu wa kidato cha sita  wamejipanga na kujiandaa  vema katika Mtihani wao wa Mwisho unaotarajiwa kufanyika tarehe  6 may 2024.


Mwl Kisha,ameongeza kuwa Shule hizo zinatoa zawadi na nafasi za kusoma bure kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika madarasa ya mitihani yaani anayefahuru vizuri darasa la 7 anapata nafasi ya kusoma bure kidato cha 1hadi 2 na anayefahuru vizuri kidato cha 2 anasoma bure kidato cha 3 hadi 4 na  anayefahuru vizuri kidato cha 4 anasoma bure kidato cha 5 hadi 6,huku wahitimu wa kidato cha sita  wanaofahuru kwa kupata daraja la kwanza Alama 3 yaani Division  1.3 kwa masomo matatu katika Mchepuo wake atapata motisha ya shiling Milioni  5 kwa kila Mwanafunzi.


Nae Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo Bi Ruth Zaipuna amewapongeza wazazi ,walezi na wanafunzi kwa  ushirikiano  mzuri uliofanya watoto wao waweze kuhitimu kidato cha sita na kuwasihi wazazi kuendelea kuwanoa na kuwapika na kuwa nguzo yao ya karibu na kuwa msingi katika kutimiza ndoto zao pia amempongeza mhasisi wa shule hizo Bw Yusto kwa kufanya ziwepo shule zote mbili Kaizirege na Kemebos.


" Ni wakati wa kujivunia kuwepo kushule hizi na nimesikia Bw Yusto kuna Muda anaendesha Gari kuwafuata na kuwarudisha wanafunzi  makwao hili ni jambo jema sana na ni unyenyekevu ,Nidhami ,Heshima ya hali ya juu sana kwenu wanafunzi na wazazi jamani tambua huyu ndiye mwenye shule lakini anaendesha gari kuwapeleka wanafunzi ,amesema Bi Ruth "


Amewasisitiza wahitimu kuendelea kujifunza kwa kila kitu pamoja na kubuni fani mbalimbali  katika jamii na kusema kwa sasa mambo yanabadilika na kugunduliwa kila siku pia na kukuwa kwa teknolojia na kuja mambo mengine mapya na bora zaidi hivyo ni vema kuendelea kujifunza bila kuchoka.


Katika hilo Bi Ruth amewasihi wazazi na walezi kuwafundisha watoto namna ya kuzifahamu fedha wakiwa wadogo na kusema kuwa wakipata elimu ya masuala ya fedha wataweza kuendesha maisha yao bila kuwa tegemezi ,kuweka bajeti zao nzuri na kuweza kuwekeza katika maisha yao ya baadae.


Amesema kuwa Bank ya NMB imeanzisha jukwaa la vijana kwa ajili ya kuwapatia elimu ya fedha na huduma mbalimbali zinazohusu vijana ,na kuwasihi kujiunga na huduma hiyo ili kupata elimu ya fedha itakayowasaidia katika maisha yao,Lakini pia amesema katika kuunga mkono sekta ya elimu NMB inatoa motisha ya kuwasomesha bure wanafunzi wanaofanya vema kwenye masomo na wale wanaotoka katika familia zenye uhitaji.


Nao baadhi ya wazazi na wahitimu akiwemo Zubeda Kinono na Alvin Kamugisha wameupongeza uongozi wa shule hizo kwa kipindi chote wakiwa shuleni hapo na kuomba kuendelea kutatua changamoto  ndogo ndogo zinazoweza kujitokeza kwa wanafunzi waliobaki shuleni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS