Kiwanda cha marumaru cha Goodwill na kampuni ya Sapphire zimetoa msaada wa vyakula na mahitaji mengine ya binadamu kwa waathirika wa mafuriko wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Kassim Mchata amemshukuru Afisa Rasilimali Watu wa kampuni ya Goodwill Jerry Malandu aliyewasilisha msaada huo kwa niaba ya kampuni hizo.
“Tumepokea mifuko 70 ya unga wa Sembe yenye ujazo wa Kilogramu 50 kila mmoja, mifuko 10 ya mchele na mifuko 10 ya sabuni kwq ajili ya wananchi wa Rufiji ambao wana wakati mgumu kwenye maisha yao baada ya kukumbwa na mafuriko” amesema Mchata.
Tangu kuanza kwa mvua za El Nino maeneo mbalimbali nchini yamekumbwa na mafuriko huku serikali ikitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko nchi nzima
0 Comments