Header Ads Widget

HELIKOPTA YA JESHI YAANGUKA YAWAKA MOTO

 


Helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) imeanguka na kuwaka moto katika eneo la Sindar kwenye mpaka wa Kaunti za Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet leo Alhamisi Aprili 18, 2024.


Vyombo mbalimbali vya habari nchini humo vimeripoti ajali hiyo ambayo watu watano wamefariki dunia huku watatu wakijeruhiwa.


Tovuti ya Nation imesema walionusurika wamekimbizwa hospitali na ndege nyingine ya Jeshi la KDF, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Marakwet Peter Mulinge amethibitisha tukio hilo.


Inaelezwa kulikuwa na chopa tatu zilizokuwa zinaondoka katika eneo hilo na yenyewe ilikuwa ya kwanza kupaa kabla ya kuanguka dakika chache.


Kulingana na ripoti, helikopta hiyo ilikuwa ikipaa kutoka Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Cheptuel.


Timu hiyo ilikuwa imeondoka kwenye mkutano uliokuwa umeitishwa kujadili hali ya usalama katika eneo la Pokot Magharibi na viongozi kadhaa wakuu walikuwamo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS