Header Ads Widget

EVERTON KUKATWA POINT TENA LIGI KUU ENGLAND (EPL).


JINAMIZI la kukatwa pointi limeendelea kuiandama klabu ya Everton ya England baada ya klabu hiyo kukatwa point 2 tena kwenye msimamo wa Ligi kuu England (EPL) baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za fedha katika uongozaji wa vilabu (FFP).

Jarida la The Athletic linaripoti kuwa miamba hiyo ya jiji la Liverpool imepokwa pointi nyingine mbili na kuifanya iporomoke hadi nafasi ya 16 kwenye msimamo, ikiwa alama mbili tu kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja.

Hapo awali, Ligi Kuu England iliipokonya Everton alama 10 lakini ikapunguziwa adhabu na kurudishiwa alama 4 kwa kilabu. Kwa ujumla kikosi hicho kinachonolewa na Sean Dyche imekatwa pointi 8 msimu huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI