Wakati mfungo wa mwezi wa Ramadhani unapofikia tamati, Waislamu kote ulimwenguni wanajiandaa kwa ajili ya Eid al-Fitr, "sikukuu ya kufuturu".
Kwa mujibu wa hesabu za unajimu, mwezi wa Ramadhani unatarajiwa kudumu siku 30 mwaka huu, na kuifanya siku ya kwanza ya Eid nchini Saudi Arabia na nchi nyingi jirani kuwa Jumatano, Aprili 10.
Siku ya kwanza ya Eid al-Fitr huamuliwa kwa kuonekana kwa mwezi mpevu unaoashiria kuanza kwa mwezi wa Shawwal, mwezi wa 10 wa kalenda ya Kiislamu (Hijri).
Miezi ya mwandamo huchukua kati ya siku 29 na 30 kwa hivyo Waislamu kawaida hulazimika kungoja hadi usiku kabla ya Eid kuthibitisha tarehe yake kamili.
Baada ya sala ya kutua kwa jua Jumatatu,(Ishaa) Aprili 8, siku ya 29 ya Ramadhani , watazamaji wa mwezi wataelekea magharibi wakiwa na mtazamo wazi wa upeo wa macho kwa mtazamo wa kwanza wa mwezi mpevu. Ikiwa mwezi mpya unaonekana, basi siku inayofuata itakuwa Eid, ikiwa sio, basi Waislamu watafunga siku moja zaidi kukamilisha mwezi wa siku 30.
Nchi nyingine hufuata mionekano huru ya mwezi.Muandamo huo unapothibitishwa, Eid inatangazwa kwenye televisheni, vituo vya redio na misikitini.
Waislamu wanasherehekea vipi Eid?
Kuanzia zamani, Eid husherehekewa kwa siku tatu kama likizo rasmi katika nchi zenye Waislamu wengi. Hata hivyo, idadi ya siku za likizo inatofautiana na nchi.
Waislamu wanaanza sherehe za Eid kwa kushiriki ibada ya maombi ambayo hufanyika muda mfupi baada ya alfajiri, ikifuatiwa na mahubiri mafupi.
Wakiwa njiani kuelekea kwenye swala hiyo, ambayo kwa kawaida hufanyika katika eneo la wazi, Waislamu husoma takbeerat, wakimsifu Mungu kwa kusema “Allahu Akbar”, kumaanisha “Mungu ni mkubwa”.
Ni desturi kula kitu kitamu kabla ya sala, kama vile biskuti zilizojaa tende zinazojulikana kama maamoul huko Mashariki ya Kati. Tamasha hili mahususi linajulikana kama Eid "tamu" - na usambazaji wa peremende ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa KiislaKwa kawaida Waislamu hutumia siku nzima kuwatembelea jamaa na majirani na kupokea peremende wanapozunguka nyumba hadi nyumba.
Kila nchi ina vyakula na peremende za kitamaduni ambazo hutayarishwa kabla ya Eid au asubuhi ya siku ya kwanza.Watoto,huvaa nguo mpya, hutolewa zawadi na pesa ili kusherehekea tukio hilo la furaha.
Wasichana na wanawake katika nchi nyingi hupamba mikono yao na henna. Sherehe ya Eid huanza usiku unaotangulia huku wanawake wakikusanyika katika vitongoji na mikusanyiko mikubwa ya familia kwa upakaji wa hina.
Salamu za Eid za kawaida ni zipi?
Salamu maarufu zaidi ni “Eid Mubarak” (Eid Njema) au “Eid sa’id” (Eid nzuri). Salamu za Eid pia hutofautiana kulingana na nchi na lugha.
0 Comments