wakili Moses Ambindwile wa tatu kulia akiwa na wananchi wa Igeleke kwenye tukio la mkazi wa eneo hilo kuuwawa.
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
KUFUATIA tukio la Kinyama la mwanamke Lukia Sanga mkazi wa Igeleke A Mjini Iringa kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ,wakili Moses Ambindwile ambae ni mkazi wa eneo hilo ataka jamii kuacha kuchukua sheria mkononi.
Wakili Ambindwile alisema leo wakati akihojiwa na Matukio Daima Media iliyofika eneo la tukio ,kuwa tukio hilo ni la kinyama na kuwa jamii haipaswi kuendelea kufanya unyama huo.
Wakili Ambindwile ambae ni mmoja wa makada wa CCM watia nia jimbo la Iringa mjini ambae alijumuika na wananchi hao katika eneo hilo kwani ni jirani na nyumbani kwake.
Marehemu Lukia Enzi za Uhai wakeTukio hilo la kusikitisha limetokea mapema asubuhi ambapo mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa chini umejaa damu , huku majeraha makubwa yakionekana kichwani.
Akizungumza na Matukio Daima TV Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kihesa Kilolo Histoni Kalumba amesema alipokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema waliomjulisha kuhusu tukio hilo.
“Majira ya saa kumi na mbili asubuhi nilipigiwa simu na wasamaria wema kwamba kuna mama mtaani kwangu ameweza kuuawa japokuwa walikuwa hawajalithibitisha hilo nilimtafuta mjumbe wa eneo hilo, naye akanieleza kuwa yupo njiani kuelekea huko, nami nikachukua usafiri na kufika eneo la tukio Nilimkuta mama huyo akiwa amekatwa kichwani na damu nyingi zikiwa zimemwagika.”
Kwa upande wake, Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Kihesa Kilolo, Robert Simoni, amelaani vikali tukio hilo na kuwataka wananchi kuepuka tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
“Mtaa wetu una ulinzi shirikishi wa vijana wanaofanya doria usiku, lakini kwa tukio hili tunalaani vikali. Sio haki mtu kuchukuliwa maisha kwa njia hii Tunaomba wananchi kuwa makini na kushirikiana kutoa taarifa kwa vyombo husika badala ya kujichukulia sheria mikono.
Pia ndugu na majirani wa marehemu wameeleza kusikitishwa na tukio hilohuku wakielezea jinsi walivyomfahamu Lukia kama mtu aliyekuwa akiishi kwa amani na majirani zake.
Akizungumza kwa masikitiko, Maria Ndongwa, ndugu wa marehemu amesema
“Mimi nilikuwa nimelala, nikaamshwa na kuambiwa kuwa mama anashida na nilipofika, nikakuta watu wamejaa wakizunguka nyumba, ndipo nilipogundua kuwa tayari amefariki.
Kwa upande wake, jirani wa marehemu ambaye pia ni wakili, Moses Abwindwile, amesema tukio hilo ni kielelezo cha hatari iliyopo katika jamii na ameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi zaidi katika maeneo ya makazi.
“Tukio hili linaonesha jamii inapaswa kuchukua tahadhari kubwa na tunaiomba serikali kupitia Jeshi la Polisi kuongeza ulinzi, kwani haya ni matukio yanayoweza kuzua hofu kwa wananchi”
Kwa upande wake Mkaguzi wa Polisi wa Kata ya Mkimbizi, Afande Daniel, amesema ulinzi ni jukumu la kila mwananchi na ametoa wito kwa jamii kushirikiana kwa karibu katika kubaini viashiria vya uhalifu.
“Suala la ulinzi ni la wote tumekuwa na vikundi vya ulinzi kama sungusungu, lakini si kila tukio linaweza kuzuiwa. Ni muhimu kupeana taarifa kwa haraka pale mtu anapohisiwa kuwa na nia mbaya Pia tusiwe tunakaa peke yetu, tuishi kwa kujaliana,”.
Naye Msaadizi wa Mkuu wa upelelezi wilaya ya iringa Afande Mtubia, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi katika kufanikisha upatikanaji wa haki.
‘’Jambo kubwa linaloweza kufikisha mwisho mambo hayo basi ni taarifa kwasababu mambo kama haya yanatokea kwa jamii zetu na sisi majirani ndo watu wa kwanza ambao tunakuwa na taarifa za mambo haya lakini pia kama kuna migogororo katika maeneo yetu basi ipo namna ya kuweza kusuluhisha mambo haya na sio kuchukua sheria mkononi kwasababu kama mtu akakaa kimya kitu kinachojengeka ni kisasi katika jamii zetu na mimi niwaombe tena kama kuna mtu au watu au taarifa yoyote kuhusiana na jambo hili basi ni vizuri tupeane taarifa wakati serikali inaendela na uchunguzi na pia wazazi tujifunze kutengeneza kizazi chenye hofu ya Mungu.
Mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea kufanyika ili kubaini wahusika



































0 Comments