Na Ashton Balaigwa,MOROGORO
SERIKALI imetoa Sh bilioni 1.3 kwa Wilaya ya Kilosa iliyopo Mkoani Morogoro,kwaajili ya kufanya utekelezaji wa miradi ya Dharua ya ujenzi wa mifereji ya kisasa, miundombinu ya Barabara za vijiji na kuboresha kingo za mito ili kumaliza tatizo la mafuriko ya mara kwa mara yanatokea katika wilaya hiyo kongwe ya Kihistoria.
Akizungumza wakati ukaguzi na kutembelea miradi hiyo huku akiongozana na Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo kama utekelezaji wa Ilani Mbunge wa Jimbo la Kilosa Profesa Paramagamba Kabudi,amesema tayari serikali alisema fedha hizo zitasaidia kuimarisha miundombinu ambayo awali ilikuwa haipo na kusababisha maji kuingia kwenye nyumba za wananchi na kusababisha mafuriko.
Profesa Kabudi amepongeza hatua hiyo ya serikali ya kutoa fedha hizo na kwamba sasa itakuwa mkombozi kwa wakazi wa Kilosa kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakiathiriwa na mafuriko hayo hata pale mvua zisiponyesha katika wilaya hiyo na kunyesha mikoa mingine kutokana na mito mingi kupita katika wilaya hiyo.
“ Kwa dhati kabisa namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha hizi kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo mifereji ya kisasa kabisa ,hii itatusaidia kuondokana na hali ya mafuriko”alisema Mbunge Profesa Kabudi….
Amesema Jiographia ya mji wa Kilosa imezungukwa na Milima na mito mikubwa, hivyo imekua ni vigumu kuepukana na mafuriko tangu enzi za wakoloni hawa hivyo ujenzi wa miundombinu hiyo itasaidia kumaliza tatizo hilo la mafuriko.
“ Sasa historia inakwenda kuandikwa, Baada ya Serikali kutenga zaidi ya shilingi bilioni 1.3 ili kujenga mifereji ya kisasa katika maeneo hatarishi” amesema Kabudi
Akizungumzia mkakati wa wilaya hiyo kuondokana na mafuriko hayo, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara wa Vijijini na Mijini(Tarura)wa wilaya ya Kilosa,Mhandisi Wiston Munyaga,amesema kuwa fedha hizo zitajenga mifereji ili kuondoa adha ya maji yanayotokana na mito mbalimbali inayosababisha mafuriko yanaingia kwenye makazi ya watu.
Naye Diwani wa Kata ya Mvumi wilayani humo,Shaban Malingo,meisema mafuriko yanayotokea wilayani yamekuwa yakigharimu maisha ya watu pamoja na makazi yake.
Mwisho
0 Comments