Header Ads Widget

WADAU WA MAHAKAMA WAFUNDWA KESI ZA WATOTO

 

Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma Augustino Rwizile  akizungumza wakati akifungua mafunzo ya wadau walio mstari wa mbele katika kushughulikia mashauri ya watoto mkoani Kigoma
wadau walio mstari wa mbele katika kushughulikia mashauri ya watoto mkoani Kigoma wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kushughulikia haki za watoto wanapoendesha mashauri mahakamani

Edna Lutengano Afisa ulinzi na usalama wa watoto UNICEF akizungumza katika mafunzo kwa wadau Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma Augustino Rwizile  akizungumza wakati wa mafunzo ya wadau walio mstari wa mbele katika kushughulikia mashauri ya watoto mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma Augustine Rwizile ametaka wasimamizi wa kesi za watoto kuzingatia haki za mtoto kulingana na sheria na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za Watoto wanaposhughulikia mashauri ya watoto mahakamani.

 

Jaji Rwizile ametoa kauli hiyo akifungua mafunzo ya siku tano kwa washiriki 64 wa mafunzo ya wadau walio mstari wa mbele katika kushughulikia mashauri ya Watoto mafunzo yanayohusisha mahakimu wa mahakama za wilaya,waendesha mashitaka,  maafisa ustawi wa jamii na wasaidizi  wa sheria kutoka taasisi mbalimbali mkoani Kigoma.

 

Alisema kuwa uendeshaji wa mashauri yam toto yamekuwa na tofauti kubwa katika uendeshaji wake kulinganisha na mashauri mengine hivyo kumekuwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa wadau kwenda pamoja katika kusimamia mashauri hayo hasa Watoto wanaokinza na sheria.

 

 

Katika mafunzo hayo yanayoendeshwa na chou cha uongozi wa mahakama Lushoto kwa ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) Jaji Rwizile alisema kuwa chochote kinachofanywa katika kusimamia mashauri hayo kitapaswa kuzingatia sheria za nchi, sheria za kimataifa na mikataba ya kimataifa ya kumlinda mtoto ambayo Tanzania imeridhia.

 

Akizungumzia mafunzo hayo Afisa ulinzi na usalama wa mtoto kutoka UNICEF, Edna Lutengano alisema kuwa bado kumekuwa na changamoto kubwa kwa wadau wote katika kusimamia mashauri ya Watoto mahakama wengi bado hawajui sheria na taratibu za kumlinda mtoto hasa wanaofanya makosa hivyo wadau wengi wanataka Watoto hao kushughulikiwa kama wahalifu wengine.

 

Lutengano alisema kuwa Pamoja na changamoto kushughulikia Watoto wenye makosa lakini bado zipo changamoto kwa kesi za Watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili kwa kesi kuishia polisi n ahata zikifika mahakamani zinaisha katika mazingira ambayo hayatoi haki kwa mtoto inavyostahili hivyo mafunzo hayo yameandaliwa kuwafundisha wadau hao kujua haki za Watoto na namna ya kusimamia mashauri kulingana na haki hizo.

 

Nestory Kulula Wakili wa serikali kutoka ofisi ya Taifa ya Mwendesha mashitaka mkoa Kigoma alisema kuwa bado changamoto ipo kwa wadau wanaofungua mashitaka dhidi ya Watoto hivyo kutaka Watoto hao kushughulikiwa kama watu wengine wakati kuna tofauti kubwa ya uendeshaji wa kesi hizo.

 

Wakili huyo wa serikali alisema kuwa kutokana na shinikizo kutoka kwa wadau wanaofungua mashitaka wakati mwingine imewafanya wasimamizi wa mashauri ya Watoto kutoa hukumu ambazo hazizingatii haki za kumlinda mtoto hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuwajenga wadau wote kutekeleza majukumu yao kulingana na sheria zinazomlinda mtoto.

 

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI