JUMUIYA ya Umoja wa vijana Uvccm imesema itawashughulikia watakaojitokeza ndani ya chama cha mapinduzi CCM kuchukua fomu kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu 2025.
Jumuiya hiyo imewaomba wanaccm kumuachia Mhe.Rais ambae ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dk,Samia Suluhu Hassan awe mgombea pekee atakaepeperusha bendera ya CCM ngazi ya urais katika uchaguzi huo.
Akizungumza na wananchi wilayani kilolo mkoani Iringa katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni ya ‘’jiandikishe chagua ccm’uliofanyika kata ya Nyalumbu, mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Muhsin Ussi alieleza kuwa kutokana na kazi na kasi kubwa ya maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Dk.Samia Suluhu Hassan hakuna sababu ya mwanccm kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea urais.
Alisema katika nafasi ya Rais vijana wa UVCCM wameweka msimamo wao kuwa fomu itakayotoka ni moja ambayo ataichukua Dk.Samia hii inatokana na kazi kubwa anayoifanya katika kipindi kifupicha miaka mitatu.
Alisema atakaethubutu kuchukua fomu ataiona rangi ya umoja wa vijanawa CCM unaoongozwa na Mwenyekiti wake Mohamed Kawaida akajitokeza kuchukua fomu.
Akimkaribisha Mgeni rasmi,Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa Agrey Tonga alieleza kuwa vijana wote wenye sifa na vigezo wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu kugombea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Toga alieleza kuwa UVCCM itawaunga mkono vijana wote watakaogombea katika uchaguzi huo na uchaguzi wa Serikali za mitaa ili kujenga uwakilishi wa vijana katika maamuzi ya Taifa na kuleta maendeleo endelevu.
Nae Mwenyekiti wa uvccm wilaya ya kilolo Amani Mdeka alisema kuwa Uvccm imejipanga kuhakikisha katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu chama cha Mapinduzi CCM kinashinda kwa kishindo mitaa yote.
MWISHO.
0 Comments