Header Ads Widget

SHULE YA MSINGI MAPUNDUZI B SHINYANGA INAUHABA WA MATUNDU YA VYOO 50, WANAFUNZI HAWANA CHOO COWOCE KUSHIRIKIANA NA WANANCHI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamati maalum ya ujenzi wa  Choo katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, kwa kushirikiana na wazazi,  leo imezindua rasmi ujenzi wa matundu matatu ya vyoo  na chumba maalum kwa ajili ya wasichana  katika shule hiyo iliyopo katika  Manispaa ya Shinyanga.

Katika taarifa yake Mwenyekiti wa kamati hiyo Mwalimu James Msimbang’ombe amesema tayari maandalizi ya awali yamefanyika na ujenzi umeanza kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na shirika la COWOCE.

Mwenyekiti wa mtaa huo kata ya Ngokolo Bwana Chief Thomas Ng’ombe amewasisitiza wananchi kushiriki vema kwenye ujenzi huo ili kupunguza changamoto ya Vyoo katika shule ya Mapinduzi B.

Akizungumza mratibu wa ujenzi huo kutoka shirika la Companion of Women and Children Empowerment (COWOCE) Bi. Grace Moses amesema shirika hilo linatekeleza mradi wa hisani kwa jamii ambapo amewaomba wananchi na wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi hizo ikiwemo kushiriki katika shughuli ya ujenzi huo.

“Katika mazingira haya ugonjwa wowote ule ukilipuka watoto wetu watakuwa kwenye ile hali ya hatari zaidi lakini leo tunazindua mradi wetu huu wa hisani kwa jamii niwaombe wananchi tujitoe, kwa mioyo yetu yote tujitoa kwa nguvu zetu zote tukisema kwamba tunajitaji nguvu kazi wananchi niwaombe kweli nguvu kazi ionekane siku hizi mpaka wanawake wanabeba Zege kwahiyo jamani tujitahidi tushirikiane tushikamane hili suala linahitaji nguvu ya pamoja”.amesema Grace

Baadhi ya wananchi waliojitokeza leo kwenye uzinduzi wa ujenzi huo wamelishukuru shirika la COWOCE huku wakiahidi kushiriki kikamilifu kwenye shughuli hiyo ya ujenzi.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Mapinduzi B, Mwalimu Japhet Jasson ameeleza kuwa pamoja na ujenzi wa matundu hayo ya Choo, bado changamoto ni kubwa kwani matundu ya vyoo yanayohitajika ni 50, na sasa yaliyopo ni 02.

“Nitoe shukurani za dhati kwa shirika la COWOCE, kupitia Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kutoa kibali kwa shirika hili kuendelea na utaratibu huu na mimi mkuu wa shule nitaendelea kuwapa ushirikiano”.

“Changamoto hii ya matundu ya Vyoo niya muda mrefu mimi nimehamishiwa hapa nikaikuta ambapo wanafunzi waliopo kwa sasa ni 1089, watoto wa kiume wanahitaji matundu ya Vyoo 22 na watoto wa kike wanahitaji matundu ya Vyoo 28 ambayo jumla ni matundu 50, na mpaka sasa hivi ninavyoongea matundu yaliyopo ni mawili tu ya wasichana nayo yalikuwa ya walimu baada ya kuona kuna uhaba wa matundu ya Vyoo walimu wakawa wamewapatia wanafunzi wa kike kwahiyo watoto wa kiume mpaka sasa hivi hawana hata tundu moja la Choo wenyewe wanajisaidia haja zao pembeni”. Amesema Mwalimu Japhet

Ujenzi wa matundu matatu ya Vyoo  na chumba maalum kwa ajili ya wasichana  katika shule ya msingi Mapinduzi B kata ya Ngokolo  Manispaa ya Shinyanga unatarajiwa kukamilika Mwezi Julai Mwaka huu 2024.

Mwenyekiti wa kamati maalum ya ujenzi wa Choo katika shule ya msingi Mapinduzi B,  Mwalimu James Msimbang’ombe akipokea michango kwa wananchi walioguswa kujitolea ili kufanikisha ujenzi huo.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI