Header Ads Widget

SERIKALI KUPELEKA VIFAA TIBA JENGO LA MAMA NA MTOTO KIBENA HOSPITALI NJOMBE

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala sheria na katiba mwenye kofia Mhe.Joseph Mhagama akiwa na Naibu waziri wa  Utumishi na utawala Mhe.Ridhiwani Kikwete katika Hospitali ya mji wa Njombe KibenaNa Gabriel Kilamlya Matukio Daima APP NJOMBESerikali imeahidi kupeleka mashine ya Kuongeza joto kwa watoto wanaozaliwa kabla ya umri pamoja na vifaa tiba vingine katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena baada ya kukamilika kwa jengo la Mama na  mtoto lililojengwa kupitia mradi wa TASAF na serikali.Akizungumza akiwa katika Hospitali hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala katiba na sheria Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Utumishi na utawala bora Ridhiwani Kikwete amesema serikali italeta vifaa tiba hivyo vitakavyowasaidia akina mama wanaojifungua na watoto wao.Aidha Kikwete amesema kwa mujibu wa ripoti mkoa wa Njombe unaongoza kwa vifo vya watoto kwa ugonjwa wa Nimonia kutokana na baridi kali hivyo ni lazima wapeleke mashine ya kuongeza joto kwenye chumba cha akina mama wanaojifungua watoto walio chini ya uzito na umr[ Inccubeter na hita]ili kupunguza baridi.Jengo hilo tayari limeshaanza kutumika ambapo Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe  Dokta Jabir Juma amesema kwa sasa nafasi imekuwa kubwa katika jengo hilo na akina mama wanapata huduma kwa urahisi.Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala katiba na sheria Joseph Mhagama na Mbunge wa Madaba mkoani Ruvuma amesema miradi ya TASAF Katika maeneo mengo imekuwa mizuri na inayojibu mahitaji ya watanzania kwani kujengwa kwa mradi huo mkoani Njombe kutasaidia kupunguza changamoto ya vifo vya watoto vinavyotokana na baridi kali inayosababisha ugonjwa wa Nimonia.Baadhi ya wananchi na akina mama walioajifungua na kutumia jengo hilo akiwemo Malkia Mligo,Agnes Mgaya na Irine Gwivaha wameshukuru kujengewe jengo hilo ambalo limekuwa mkombozi kwa wanawake na watoto huku wakiomba kusaidia ukarabati wa miundombinu mingine.Jumla ya shilingi Milioni 160 zimetumika kujenga jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya mji wa Njombe Kibena  ambapo kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 150 zilitolewa na Tasaf huku nyingine zikitolewa na halmashauri,Wananchi na mkuu wa wilaya ya Njombe.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI