Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mutunzi Ishabailu (52) amefikishwa Mahakamani akikabiliwa na tuhuma ya Uhujumu Uchumi.
Mawakili wa Serikali Yese Temba na Felix Mashama Februari 29,2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mara Erick Marley walisema mshitakiwa anakabiliwa na makosa matatu ya kughushi.
Wakisoma hati ya mashitaka katika kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 20240229200005408 walisema, Juni 20,2023 mshitakiwa alighushi kwa kuutumia komputa na kujipatia Sh 213,748,085 .
Wamesema,tarehe hiyo mshitakiwa alitenda kosa la kutatisha fedha haramu na kusababishia mamlaka hasara.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za Uhujumu mpaka Mahakama Kuu.
Mshitakiwa yuko mahabusu na kesi hiyo itatajwa tena Machi 14,2024.
Februari 27,2024 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Madiwani na watumishi halmashauri ya wilaya ya Serengeti alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Salum Morcase amkamate Ishabailu na DPP afungue mashitaka haraka Mahakamani.
Alisema, mweka hazina huyo kwa kushirikiana na watumishi watatu wa kitengo cha Treasure Single Account (TSA) waliiba fedha hizo
Na Juni 21,2023 Ishabailu alifanya matumizi ya fedha hizo kwa kushirikiana na mfanyabiashara Daud Matinde,kupitia akaunti zake za NMB na CRDB aliweka miamala minne kwa nyakati tofauti.
Na alimtaka azitoe kwa kuwa ninatakiwa kwa ajili ya kazi ya haraka,na alifanikiwa kutoa sh 189milioni na kumkabidhi na kubaki na sh24,748,085 aliweka ndani ya begi na kuzisafirisha kwa njia ya basi hadi Stendi Nyegezi na kumkabidhi Zablon ambaye ni miongoni mwa ambao wanadaiwa watumishi wa Tamisemi Dodoma waliokwisha kamatwa na kufikishwa Mahakamani.
#Chanzo:Serengeti Media Centre -Mara
0 Comments