Header Ads Widget

ACT WAZALENDO WAONYWA KUTISHIA KUJITOA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

 

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

KUFUATIA Chama cha ACT Wazalendo kutangaza  hadharani dhamira yao ya kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa kile wanachodai kutotekelezwa kwa hoja zao, Wadau wa Siasa akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini Ameir Hassan wametaka  chama hicho kuacha Mara moja  kufanya siasa zilizopitwa na wakati badala yake wafuate sheria na utaratibu wa kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama katiba ya Zanzibar  inavyoeleza.


Ameir amesema, Katiba inaeleza utaratibu wa kujitoa katika serikali ya umoja wa kitaifa hivyo kama wanahitaji kujitoa wanapaswa wafuate sheria kuliko kutishia na kupelekea taharuki kwa Wananchi.


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini Ameir ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Tunguu wakati akitoa salamu za kuukaribisha  Mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka 2024 miladia sawa na mwaka 1445 Hijiria.


Amesema kuwa, kinachofanywa na chama cha Act Wazalendo ni siasa za chuki, siasa za fitna na siasa zilizopitwa na wakati.


"Katiba ya Zanzibar ibara 42(a) inaeleza utaratibu mzima wa kuwepo na kujitoa katika Serikali ya umoja wa Kitaifa hivyo kama kweli wao wamedhamiria kujitoa wanapaswa kufuata taratibu huo kuliko kutangaza kwenye vyomb vya habari na kuleta taharuki kwa Wananchi," amesema.


"Ukweli kwamba, hawana sababu ya kuzungumza na vyombo vya habari,  hawana sababu ya kuongea na Rais Samia, hawana sababu ya kuongea na Rais Mwinyi wanatakiwa kufuata utaratibu ukizingatia wanawanasheria," ameongeza.


"Makamu wa Kwanza Othman Masoud ni mwanasheria nguli sana hivyo tunamuomba atumie sheria kwa maslahi ya Wazanzbar na asitumie sheria kisiasa, asitume sheria kwa maslahi na chama chake tu," ameeleza.


Aidha Ameir amedai kwamba kinachofanywa na chama cha Act Wazalendo ni hujma na  dhidi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kukosa ajenda kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.


Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo amemuomba Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shabaani kufanya ziara maalum katika maduka na  masoko ili kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais wa Zanzibar la kutopandisha bei za bidhaa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.


"Waziri anapaswa kuandaa ziara za kutelembelea maduka na masoko kufuatilia agizo la Rais Dk.Mwinyi la kutopandisha bei za bidhaa hususani bidhaa za chakula katika mwezi mtukufu wa Ramadhani," ameeleza.


"Mimi nasema hii Waziri wa Biashara ametoka ACT Wazalendo ametoka chama Act Wazalendo hivyo kama wameamua kujitoa basi wajite mapema ili kupisha wengine wanaoweza kufanya kazi za kumsaidia Mhe. Rais Dk. Mwinyi kwa vitendo," ameeleza Ameir Hassan.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI