Header Ads Widget

12 WAKAMATWA KWA KULA MCHANA WA RAMADHANI HADHARANI ZANZIBAR

 

Kufuatia taarifa mbali mbali zilizokua zikisamba mitandaoni zilizokua zikidai kuna baadhi ya watu hua wanatabia za kula hadharani mchana wa Ramdhani Zanzibar jeshi la polisi lilifuatilia taarifa hizo na kubaini uwepo wa watu wanaokula mchana wa Ramadhani
 
 Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa mjini magharibi (Zanzibar) ACP. Abubakar amesema walifanya msako na kuwakamata watu hao 12 waliokula hadharani kwa maeneo tofauti ya mjini na kusisitiza kua ni kosa kula hadharani wakati wa ramadhani na watu hao wanashikiliwa katika kituo hicho cha madema kwa tararibu za kupelekwa Mahakamani

 

Aidha waandishi wa habari awali kabla ya Ramadhan walifanya mahojiano maalum na mrajisi wa Baraza la Sanaa Zanzibar ambalo pia husimamia Milka ,Silka na tamaduni Zanzibar na kupiga maarufuku ya kupigwa kwa mziki ,Mabaa kua wazi na Ulaji holela wa hadhrani wakati wa Ramadhani na Uvaaji wenye staha ,katika kipindi Hiki cha Ramadhani Baadhi ya migahawa hufungwa na vyakula hupatikana sehemu maalumu zilizoruhusiwa ambapo watu huruhusiwa kula kwa kutoonekana hadharani

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS