Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp,Dar
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewataka wanachama wa Chama hicho kukataa kupokea malalamiko ya mtu yoyote anataka kuwaganya huku akiwataka waendelee na mshikamano wao wa kujenga na kukiimarisha chama chao.
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo wakati alipokua akihutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu kupitia kikao maalum ambacho kimehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 119 ambapo kimelenga kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo Katiba ya uchaguzi .
"Mtu yoyote atakaekuja kuwapa malalamiko yoyote yanayoashiria kuleta mtafaruku kwenye chama ama kutaka kutugawanya naomba musikubali na muyapuuze na tuendelee na mshikamano wetu wa kujemga na kukiimarisha chama chetu na kuyafikia malengo yetu tuliojiwekea"amesema Zitto
Amesema kuwa, Chama hicho kimeendelea kujiimarisha kitaasisi kwa kuanzisha taasisi mbili muhimu ambazo zinatekeleza malengo na madhumuni ya chama na kuhakikisha ustawi wa wanachama ambapo taasisi hizo baraza kivuli la mawaziri na shusha tanga saccos.
"kwa upande wa Baraza kivuli la Mawaziri ambalo lipo chini ya uongozi wa Waziri Mkuu kivuli, Dorothy Semu na Katibu Mkuu Kiongozi Idrissa Kwaweta lengo ikiwa ni kukosoa sera za Serikali iliyopo madarakani na kupendekeza mbadala wa sera, tumeona baadhi ya mapendekezo ambayo tunayatoa serikali wanayafanyia kazi"amesema Zitto.
Aidha, ameongeza kuwa Taasisi ya Shusha Tanga Saccos, Act Wazalendo imekua ikiendeleza nibya hiari na yawanachama wenyewe kwa ajilinya kukabiliana na changamoto za kimaisha kutokana na mambo ya mikopo yenye riba kubwa maaruf kama kausha damu.
"kutokana na usajili wa wanachama kwenye Saccos hiyo kutokua na nguvu, niwasihi wajumbe wa Halmashaur Kuu ya Chama Taifa kwanza nyinyi wenyewe muwe mfano kwa kujiunga ili kuonesha njia ya kuhamasisha wanachama wengine"amesema Zitto.
Aidha amesema kuwa,wamefanikiwa kuchagua uongozi katika majimbo yote 264 nchi kote ambapo majimbo 214 ni ya Tanzania bara na 50 Zanzibar, huku mikoa yote ikichagua viongozi wake jambo ambalo ni ishara ya ukuaji na nguvu ya chama hicho.
Sambamba na hayo, kuna masuala mahususi ambayo yasipochukuliwa hatua yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa taifa ikiwa ni pamoja na migogorobya ardhi na migogoro ya mipaka kati ya hifadhi na vijiji,kupanda kwa gharama za maisha.
"Chama chetu kinaendelea kutoa wito kwa Serikali kutimiza wajibu wake huo kwa kupitia baraza Kivuli la Mawaziri tumekuwa tukitoa majawabu ya hatua zinapopaswa kuchukuliwa, Serikalu kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kuongeza tija kwa mkulima"amesema Zitto
Aidha, ameongeza kuwa walipeleka mapendekezo 10 ya miswada bungeni ambapo 6 yamechukuliwa, hivyo wanajipa moyo kuwa mabadiliko hayo ni hatua muhimu sana katika safari yao ya kudai chaguzi huru na zenye haki na kuacha alama ya kudumu katika nchi kupitia chama chao.
"Miswada ilikua na mambo mengi sana chama chetu kupitia kamati kuu yetu ya chama tulichambua na kupendekeza mambo 10 mahususi ya kuyabeba na kuyawasilisha bungeni, kati ya mambo 10 tuliopendekeza 6 yamechukuliwa kama yalivyo na kuwekwa katika sheria hizo mpya"amesema Zitto.
0 Comments