Header Ads Widget

WATUMISHI TAWIRI WAPATA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA MANUNUZI YA UMMA (NeST)






Wakuu wa Idara/Vitengo pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)  wanashiriki mafunzo ya Mfumo mpya wa kielektroniki wa Manunuzi ya Umma  (_National e-Procurement System of Tanzania - NeST_) ambao ni mbadala wa mfumo wa awali  wa Tanzania National e Procurement System yaani (TANePS).


Dkt. Janemary Ntalwila  akimwakilisha Mkurugenzi  Mkuu  TAWIRI, ametoa wito kwa watumishi hao kuzingatia mafunzo hayo  yenye tija katika manunuzi ya umma "zingatieni mafunzo na kufanya majaribio  zaidi "amehimiza Dkt. Ntalwila 


Bw. Japhet Laizer ambaye ni miongoni mwa wakufunzi wa mafunzo hayo, amesema mfumo wa NeST  ni Mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma umelenga kutatua changamoto  za mfumo wa awali wa Taneps .


Aidha, Laizer ameeleza  NeST  ni mfumo bora na salama kwani umetengenezwa na Watanzania, pia ni mfumo rafiki na rahisi kwa watumishi ambao utasaidia kudhibiti rasilimali za Serikali na utazuia mianya yote ya upendeleo na rushwa katika mchakato wa manunuzi, kuharakisha utendaji  na kuongeza uwazi. 


Mafunzo haya ya siku tano yanafanyika  kwa nadharia na vitendo  katika Makao Makuu ya TAWIRI, Njiro - Arusha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI