Header Ads Widget

WAZIRI NAPE AWATAKA VIONGOZI KUTUMIA TAKWIMU ZA SENSA KATIKA KUKUZA UCHUMI

Na Matukiodaimaapp, Lindi

Waziri wa habari na Teknolojia ya habari Nape Nnauye, akimwakilisha Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,amesema kuwa Viongozi na Watendaji  watumie takwimu za sensa katika kukuza uchumi wa nchi katika kufanya maendeleo.


Mafunzo ya uwasilishwaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi katika viwanja  vya Ilulu Manispaa ya Lindi, Jumatano ambapo Waziri wa habari na Teknolojia ya habari Nape Nnauye amesema kuwa takwimu za sensa zitumike katika kuleta  maendeleo,kwa kukuza mkoa wa lindi katika uchumi .


"Viongozi wote na watendaji ambao wamepatiwa mafunzo wanatakiwa kupanga mipango ya maendeleo kwa kutumia takwimu za sensa,ili kuweza kupanga mipango ya kimaendeleo" .Amesema Waziri Nape


Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack  wakati akitoa salamu za mkoa amesema kuwa takwimu za sensa zinaonesha kuwa mkoa wa Lindi unajumla ya waakazi zaidi ya milioni 1laki 194,028.


Takwimu ya sensa ya mwaka 2022,itasaidia kupanga mipango ya mkoa  ambapo itasaidia kujua maeneo yenye changamoto.Amesema RC

 Kamisaa wa Sensa Anna Makinda ,amesema kuwa Sensa ya mwaka 2012,iliwapa shida kutokana na wananchi wengi walikataa kuhesabiwa ,ambapo  mwaka huu wananchi wote walijitokeza kuhesabiwa .

"Sensa ya mwaka 2012,ilitusumbua sana kutokana na wananchi wahakujitokeza wote kuhesabiwa ilitupa changamoto sana,ila kwa mwaka 2022,tunashukuru wote walijitokeza ."Amesema Anna


Mariamu Juma  mmoja  ,amesema kuwa  mafunzo waliyoyapata yatawasaidia  katika maeneo yao ilikuweza kutambua changamoto mbalimbali za eneo lao na kuweza kupanga mikakati mabalimbali ya kimaendeleo.


"Tunawashukuru watu wa takwimu ya sensa kwa mafunzo mazuri,ambayo yatatusaidia katika maeneo yetu ya vijijini na hata maeneo ya mjini zamani Serikali ilkuwa inashindwa kufanya mipango ya kimaendeleo kutokana na idadi sahihii ya watu haijulikana ila kwasasa maendeleo yatapatika kwa harakana kutokana na mipango mizuri".Amesema Fatuma

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS