Header Ads Widget

JANETH RITHE SASA KUGOMBEA NGOME YA WANAWAKE ACT WAZALENDO

 


NA MWANDISHI WETU MATUKIO DAIMA App, DAR


Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama cha ACT Wazalendo, Janeth Rithe ametangaza rasmi kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo Februari 9, 2024; amesema anagombea nafasi hiyo akiamini anao uwezo, uthubutu na uimara kuongoza ngome hiyo.


Rithe ambaye amekuwa Mwenezi wa chama hicho kwa mafanikio makubwa amewaasa wanachama na wanawake wa ACT Wazalendo kwamba hawatojuta endapo watampa ridhaa ya kuongoza Ngome hiyo.


"Ndugu waandishi na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. Nitumie nafasi hii kuwatangazia wanachama wa ACT Wazalendo na umma kwa ujumla kwamba Mimi Janeth Joel Rithe; ninatangaza rasmi kuwa nitagombea nafasi ya Uenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa wa chama chetu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 2/03/2024


"Ninagombea nafasi hii nikijua kabisa kwamba Ngome ya Wanawake inahitaji kiongozi mwenye uthubutu, imara, shupavu na mwenye ushawishi wa kuweza kuunganisha nguvu ya wanawake ndani na nje ya chama kwa maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla.


Niwahakikishie wanawake wa ACT Wazalendo na wanachama kwa ujumla kwamba ninagombea nafasi hii nikiamini ninazo sifa hizo. Hivyo hawatojuta endapo watanipa ridhaa ya kuongoza Ngome ya Wanawake." amesema Rithe.


Aidha kupitia taarifa hiyo; Rithe amewaalika waandishi wa habari kuhudhuria mdahalo wa wagombea wa nafasi za Ngome ya Wanawake utakaofanyika tarehe 24/02/2024.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI