Header Ads Widget

UNYWESHAJI ULANZI WATOTO WAPIGWA MARUFUKU WANGING'OMBE NJOMBE

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati Kampeni ya Lishe ikishika kasi mkoani Njombe ili kukabiliana na Udumavu mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ameonya wakazi wa wilaya ya Wanging'ombe wenye tabia ya kuwanywesha ulanzi watoto ili walale badala ya kuwapa chakula bora.


Akinyeshewa na  mvua katika kijiji cha Igwachanya wilayani Wanging'ombe kutoa elimu ya Lishe Mkuu huyo wa Mkoa Bwana Antony Mtaka amesema kitendo cha kuwanywesha ulanzi watoto pindi wanapokuwa kwenye majukumu ili walale ni kuwasababishia udumavu jambo ambalo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha Jamii wilayani Humo Imetakiwa kuondokana  na mazoea na mila zinazochangia udumavu ikiwa ni pamoja na ulevi uliyopindukia huku akisema wanatarajia  kutoa elimu hiyo makanisani,misikitini na shuleni


Wananchi wilayani Wanging'ombe akiwemo Danford Mpumilwa na Sophia Mbeyela wamekiri kuipokea vyema elimu ya lishe huku wakiahidi kwenda kuifanyia kazi.

Elimu hiyo pia imewafikia wanafunzi na walimu ambapo Amina John anaishukuru serikali kwa kuona ukubwa wa tatizo hilo na kuanza kutoa elimu huku mwalimu mkuu wa shule ya msingi Masaulwa Bahati Ndondole akisema tayari shuleni kwake ameanzisha ufugaji wa kuku wa nyama na mayai pamoja na bustani ya mbogamboga ili kutokomeza udumavu.

Kujaza tumbo sio Lishe,Jali unachokula na Unachomlisha mwanao,Ndio Kauli mbiu ya Kampeni ya Lishe katika Mkoa wa Njombe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI