Header Ads Widget

UBOVU WA BARABARA WASITISHA HUDUMA SIKU 4/WILAYA MBILI ZAKOSA MAWASILIANO

Wakazi wa wilaya ya Liwale na Nachingwea mkoani Lindi wamekosa mawasiliano Kwa siku nne baada ya kuvunjika kwa daraja linalounganisha wilaya hizo mbili eneo la Lionja B hali iliyosababishwa na kujaa maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Wananchi na wakazi wa maeneo hayo wameiomba serikali kutengeneza daraja hilo ili hali iweze kurudi kama ilivyokuwa hapo awali.

Naye mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo amefika katika eneo hilo ili kujiona adha wanayoipata wakazi hao na kuwataka kuwa wavumilivu wakati wakiandaa namna ya kushughulikia changamoto hiyo kwa haraka.

Aidha, Moyo amemtaka meneja wa Tanraods mkoa wa Lindi kufika eneo hilo Kwa haraka wakiwa na vifaa kamili na kurekebisha eneo hilo na kurejesha huduma kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI