Mwema Mungu Wetu wa Mbinguni Kila wakati tunakushukuru wewe Kwa ulinzi wako kwani pekee yetu tusingefika wakati huu.
Usiku huu tunapokwenda kupumzisha miili na akili zetu tunakuja mbele Zako Kwa unyenyekevu tukikuomba ulinzi wako usiku huu na hata utuwezeshe kuamka salama asubuhi .
Tunakemea nguvu zote za giza na Mipango yote ya mwovu shetani dhidi yetu na familia zetu tunaomba wewe Mungu utufunike mbawa za malaika Zako .
Kwani Katika kitabu Cha Nehemia 2:3 maandiko yanasema Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto?
Hivyo Mungu ni Imani yetu nyuso zetu Kamwe hazitakuwa na huzuni maana wewe u mtetezi Wetu .
Usiku huu tunakabidhi familia zetu kwako ,wagonjwa wakaione kesho iliyo njema na wenye huzuni wakapokee Faraja ,wote wanaosafiri wakavushwe salama mkono wako wa Baraka ukawashike .
Tunaomba Kwa ajili ya wote wenye mamlaka akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan,Rais wa Zanzibar Dkt Husein Mwinyi ,Waziri mkuu ,makamu wa Rais ,spika wa Bunge na wabunge wote pia mahakama zetu na wote wenye mamlaka Katika Taifa letu .
Munga baba wa Mbinguni tumeomba yote haya Kwa jina lako .
AMEN
0 Comments