Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAAP NJOMBE
Askofu mstaafu wa jimbo la Dar es salaam Kadinali Polcarp Pengo amemuapisha Askofu mpya wa jimbo la Njombe Eusibio Kyando ambaye anaanza kuhudumu katika jimbo hilo akiwa Askofu wa tatu.
Katika Uapisho huo Kadinali Pengo amemtaka Askofu Kyando kwenda kuliongoza jimbo la Njombe kwa busara kubwa kwani atakutana na vikwazo vingi.
Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu sera na uratibu wa bunge Jenister Mhagama amemuomba Askofu huyo kuendeleza miradi ya jimbo inayotoa huduma kwa wananchi ikiwemo ya Maji,elimu,Afya pamoja na kudumisha amani.
Baada ya kuapishwa na kuanza kazi rasmi ya utume katika jimbo la Njombe Askofu Kyando amewaomba wakatholiki wote waendelee kumuombea ili atende kazi ya mungu ipasavyo.
Kwa upande wao waumini wa jimbo Katholiki la Njombe wamesema sasa changamoto zilizokuwa zikikwama kwa kumkosa Askofu zitakwenda kutekelezwa huku mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika akisema viongozi wa dini ni muhimu katika kuiweka sawa jamii.
Askofu Eusebio Kyando ameanza utume katika jimbo la Njombe akiwa Askofu wa Tatu akitanguliwa na Maaskofu wawili Raymond Mwanyika na Alfred Maluma ambao wote walifariki dunia.
0 Comments