NA HADIJA OMARY
Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA Imeanza maadalizi ya kutafuta chanzo cha maji chini ya aridhi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa kata ya kilimarondo halmashauri ya Nachingwea Mkoani
Akiwa katika muendelezo wa Ziara yake ya siku mbili Mkoani Lindi Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugezi wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA Mhandisi Ruth Koya ametembelea katika kijiji cha kilimarondo na kuona uanzishwaji huo wa chanzo cha maji
Amesema amefurahishwa kuona mtambo wa uchimbaji visima tayari upo eneo la mradi tayari kwa kuanza kazi
Kwa mujibu wa Ofisa kutoka ofisi ya Bonde la Ruvuma na pwani ya kusini Mhandisi Amadeo Mkumbi amesema Kisima hicho kinataraji kuwa na urefu wa mita 150 ambapo kazi ya uchimbaji itaanza siku chache zijanzo " baada ya ofisi ya bonde kufanya utafiti tulibaini maeneo mawili ambayo yanaweza kuwa na maji ambapo tulilipendekeza eneo hili licha ya kuonekana na kuwa na mwamba mgumu lakini maji yapo ya kutosha na kazi ya uchimbaji ilitakiwa kuanza leo lakini kutokana na hali ya udogo ya hapa tumeshindwa kuanza kazi hiyo mpaka tutakapo andaa njia ya kupitisha magari yetu makubwa ya mtambo ambapo kazi hiyo inaweza kuchukua siku mbili au tatu" alisema Mhandisi Mkumbi
Kwa upande wake Mhandisi Muhibu Lubasa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Lindi amesema baada ya hatua hiyo ya kwanza ya utafiti na utambuzi wa maji kukamilika hatua inayofuata ni uchimbaji wa kisima na uanzaji wa kazi ya usanifu kisha utangazaji wa tenda kwa ajili ya ujengaji wa miundombinu
Wananchi wa kata ya kilimarondo akiwemo Betra Paul na Evodia Dickson wamesema watafarijika kuona mradi wa maji safi ukiwafikia katika maeneo yao kwani hivi sasa wanatumia maji kutoka katika mito na Mabwawa ambayo sio salama kwa afya zao
Mwisho
0 Comments