Header Ads Widget

MAVUNDE WANANCHI DODOMA CHANGAMKIENI FURSA ZA KIUCHUMI

 

Na Hamida Ramadhani Matukio Daima App Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka wajasiriamali wa Jiji la Dodoma kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo Dodoma na hasa kuzingatia ukuaji wa kasi wa Jiji baada ya maamuzi ya serikali kuhamishia shughuli zake zote Dodoma.


Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa zoezi la kugawa majiko na mitungi ya gesi 500 kwa Mama Lishe na Baba Lishe wa Jijini Dodoma.


Mbunge huyo amesema nafasi hiyo ni yakipekee ambayo wanadodoma wanapaswa kuichangamkia badala ya kuwa watazamaji wa fursa.

“Tunaishukuru Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fursa nyingi za kiuchumi zitokanazo na shughuli mbalimbali kufuatia serikali kuhamia Dodoma.


Naamini majiko haya yatachochea zaidi shughuli za kiuchumi kwa Wajasiriamali na hivyo kuboresha shughuli zao za kipato cha kila siku.

Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hivi sasa tunaandaa utaratibu wa upatikanaji wa mitambo ya kutengeneza mkaa mbadala(briquette) na kugawa kwa vikundi vya wakina Mama na vijana”Amesema Mavunde


Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amepongeza zoezi la ugawaji majiko kwa wajasiriamali huku wakisisitiza juu ya elimu ya kutosha ya matumizi ya majiko hayo ili yasilete athari baadaye.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ORYX Benoit Araman amesema Kampuni yake inaunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi kwa wananchi na kwamba wataendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi ili kutimiza lengo la 80% ya matumizi ya nishati safi kwa wananchi ifikapo mwaka 2032.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI