JESHI la polisi mkoa wa Iringa limepongeza utendaji kazi wa vyombo Vya habari mkoani hapo kuwa kazi inayofanyika ni Kubwa na jeshi hilo linategemea Ushirikiano zaidi .
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi ametoa pongezi hizo Leo wakati akifungua mdahalo wa ulinzi na usalama kwa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa ,mdahalo uliofanyika ukumbi wa NFS mjini Mafinga wilaya ya Mufindi .
Kamanda Bukumbi alisema kuwa pamoja na pongezi kwa kazi nzuri kwa wanahabari ila jeshi hilo linahimiza maadili na Misingi ya uandishi wa habari pia kujua walengwa wakuu katika wa taarifa za jeshi la polisi .
Alisema kuwa wakati vyombo Vya habari vikiwa katika mkakati wa kujenga heshima katika tasnia ni vema wanahabari kuhakikisha wanafanya kazi hiyo kwa weledi zaidi .
"Sisi tunategemea mwandishi wa habari ajue baadhi ya Sheria ili anaporipoti Kuripoti kwa kuzingatia Misingi na kujua Sheria inasemaje"
Awali mwenyekiti wa chama Cha Waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard alisema kuwa kumekuwepo na tatizo Kubwa la Ushirikiano kati ya vyombo Vya habari na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mufindi ambay
o imekuwa ikizuia Waandishi kufuatilia unyanyasaji wa wafanyakazi kwenye viwanda vyao .
0 Comments