Header Ads Widget

POLISI IRINGA WAKAMATA WATOTO 34 USIKU

JESHI  la polisi mkoani Iringa limefanya oparesheni ya kukamata watoto watoto 34 Wenye miaka kati ya 5 na 17  wanao zulula usiku kwenye kata ya Kihesa mjini Iringa .

Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wazazi na watoto waliokamatwa mkuu wa upelelezi na makosa ya ya jinai ACP Issa Suleiman alisema  oparesheni hiyo ni endelevu ndani ya mkoa huo .

" Tulishasema na si mara moja na tumefanya mikutano ya polisi jamii,na katika watoto hawa wapo wazazi waliojitokeza kuwafata watoto wao na wapo ambao hawajaja mpaka sasa" alisema

Aidha Kamanda aliwaonya wazazi na walezi kutowatuma watoto usiku kwani ni hatari akiwa peke bila uangalizi kwani  huwezi jua atakutana na vitu gani usiku akiwa mwenyewe :
Wazazi wa watoto 34 waliokamatwa wakiwa Polisi 



"Tutawasamehe lakini kwa mara nyingine hatutowaacha tutawapeleka mahakamani wazazi wote watakaozembea kwenye malezi ya watoto"

Kwa upande wa Afisa ustawi wa jamii  Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tinaeli  Mbaga, alisema jukumu la kumlinda mtoto kwa kumjibu wa sheria ya mtoto Namba 29 inaweka jukumu la Kwanza la kumlea mtoto ni mzazi hata hii oparesheni imefanyika ya kuwakamata wazazi na watoto.

"Na tunaamini kuwa kama mzazi atatimiza wajibu wake kwa mtoto basi tutapunguza matendo mengi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI