Header Ads Widget

MAKONDA KUKIWASHA TANGA JAN 20-21

Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga. 

KATIBU wa Nec,itikadi,uenezi na mafunzo toka Chama cha Mapinduzi Paul Makonda kesho Jan 20 ataanza ziara yake Mkoani Tanga ambapo atapata fursa ya kutembelea miradi ya Serikali na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi.


Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Selemani Sankwa alipozungumza na waandishi wa habari juu ya ziara ya Makonda Mkoani hapa.


Sankwa alisema ziara hiyo ya Makonda itakuwa na malengo makuu mawili ambapo atapata wasaa wa kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama hicho kama inavyofahamika mwaka 2020 Watanzania waliamua ilani ya CCM itekelezwe kwa kipindi cha miaka 5.


Alisema Ndugu Makonda akiwa kama kiongozi wa chama na ndio mwenye idara inayohusika kwa kina utekelezaji wa ilani ni wajibu wake kupita na kuona kwa namna gani miradi ya Serikali na ile ya maendeleo ambayo iliahidiwa kwa wananchi jinsi inavyotekelezwa.


Aidha alisema ukaguzi wa chama ni muhimu hasa kwa mwaka huu wa 2024 ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku ukifuatiwa na uchaguzi Mkuu 2025 wa Madiwani,Wabunge na Rais ambapo ataangalia Chama ngazi ya Mkoa jinsi kilivyojipanga na chaguzi hizo.


"Ndugu zangu waandishi wa habari ziara hii inamanufaa makubwa kwa Chama hasa kipindi hiki tunapoelekea kwenye chaguzi zilizopo mbele yetu ili kukidhi madhumuni ya kikatiba ya chama chetu ya kushinda chaguzi zote,kushika dola na kuunda Serikali"Alisema Sankwa.


Mbali na hayo Sankwa pia alisema wananchi watapewa fursa ya kutoa kero zao ingawa uongozi ngazi ya Wilaya na Mkoa wamekuwa wakifuatilia na kutatua kero za wananchi hai ingawa zipo kero ambazo zinazohitaji viongozi toka ngazi za juu.


Sankwa alisema katika ziara hiyo Jqn 20 ndugu Makonda atapata fursa ya kutembelea mradi wa daraja la Mto Pangani na kufanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa Wilaya hiyo kabla ya mkutano wake mkubwa utakaofanyika siku hiyohiyo Jijini Tanga. 


Alisema Jan 21 ziara itaendelea katika Wilaya ya Muheza, segera na kufanyika mkutano wa hadhara katika Wilaya ya Korogwe ambapo atapokea kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi papo kwa papo kama ulivyo utaratibu wake.


'Ndugu zangu bwana Makonda utaratibu wake ni kwamba zege hailali kero zote lazima zitafutiwe ufumbuzi na hui ndio mfumo wake "Alisema Sankwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI