BARUA YA WAZI KWA RAIS SAMIA
Aliyekuwa mfanyakazi wa Tanesco mkoa wa Njombe Albert kayuki amemwandikia barua ya wazi Rais Samia Suluhu Hassan akilalamikia shirika hilo kushindwa kumlipa fedha zake ambazo amekuwa akidai toka mwaka 2017 baada ya kusimamishwa kufanyakazi katika shirika hilo.
Kayuki ameelezea kuwa aliajiriwa na Tanesco Mwaka 2009 na mwaka 2017 mkataba wake ulisitishwa na kupewa barua yenye kumbukumbu no NJ/RM/PF/NO767/15-08-2017 ambayo iliambatanisha malipo yote anayostahili kulipwa.
Kupitia barua hiyo ameelezea jitihada mbalimbali alizozichukua katika kufuatilia malipo hayo ndani ya mkoa wa Njombe bila mafanikio yoyote na baada ya hapo akaandika barua ya malalamiko katika ofisi ya Rais menejiment ya utumishi wa Umma na utawala bora mara tatu huku barua hizo zikijibiwa kwa kuitaka Tanesco mkoa wa Njombe mkulipa madai yake lakini mpaka sasa hajapokea malipo yoyote.
Kufuatia hatua hiyo, Kayuki ameamua kumwandikia barua ya wazi Rais Samia Suluhu Hassan ili kuweza kupata haki yake kwani kwa kipindi chote hicho cha madai amekuwa akiugua kwa muda mrefu jambo ambalo linachangia kuwa na uhijataji wa haraka wa fedha hizo.
0 Comments