Header Ads Widget

ZITTO AKEMEA POLISI KUTEKA WANAOTUHUMIWA MASUALA YA 'KAMCHAPE

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

KIONGOZI wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amelitaka jeshi la polisi mkoa Kigoma kuacha kuteka na kutesa kwa kisingizio cha kushiriki kwenye vitendo vya Imani za kishirikina maarufu kama KAMCHAPE.

Zitto alisema hayo akihitimiza ziara yake ya siku 14 kukutana na viongozi wa chama hicho kwenye kata za zote za mkoa Kigoma na kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo manane ya mkoa Kigoma na kusema kuwa ni jambo baya jambo hilo linalofanywa na polisi.

Alisema kuwa kama kuna Ushahidi wa watu wanaokamatwa kuhusika na matukio hayo ni vizuri wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria lakini kuwakamata watu na hatimaye kutojulikana walipo ni jambo baya kwani linatesa familia.


Katika hatua nyingine Zitto  amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wanachama wao mkoani Kigoma kuungana kupigania maslahi na mustakabali wao mkoa wao na wananchi wake badala ya majukwaa ya kisiasa kutumika vibaya na kuwa kikwazo cha maendeleo ya mkoa.

Kiongozi huyo alisema kuwa ipo miradi ambayo ilikuwa itekelezwe na benki ya Dunia ukiwemo mradi wa umwagiliaji bonde la Mto Luiche ambayo ilikwama kutekelezwa wakati ACT ikiongoza manispaa na sasa baada ya jitihada kubwa mradi huo umepata idhini kutekelezwa hivyo siyo vizuri siasa kuhamishiwa kwenye kukwamisha maendeleo.

Awali Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa ACT Wazalendo, Muhonga Ruhwanya alisema kuwa chama hicho kimeipanga kuhakikisha kiongozi wao anarudi na kuchukua jimbo la Kigoma Mjini kwani kwa miaka mitano hakuna miradi ya maana iliyofanyika.

 

Muhonga alisema kuwa ACT Wazalendo kupitia viongozi na wagombea wake imeiwekea dhamira ya dhati ya kushika madaraka na kuwatetea wananchi katika kuwaletea maendeleo baada ya mkoa huo kuwa nyuma kiuchumi kwa mrefu.

 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI