Header Ads Widget

ANDENGENYE ANOGESHA TAMASHA LA TRA KIGOMA

 

Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Mcha Hassan akizungumza wakati wa bonanza la michezo lililoandaliwa na TRA mkoa Kigoma

Mkuu wa wilaya Kigoma 
Salum Kali (wa tatu) akizungumza na timu za mpira wa mguu za wafanyabiashara na watumishi wa TRA katika bonanza lililofanyika viwanja vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma
Washiriki wa bonanza la Mlipa kodi lililoandaliwa na Mamlaka ya mapato mkoa Kigoma wakiingia kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre kwa matembezi ya kilometa saba yaliyoanza ofisi za TRA mkoa Kigoma


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amefanikisha tamasha la michezo la kuhamasha ulipaji kodi kwa hiari akisema kuwa ulipaji kodi kwa hiari unafaida kubwa katika kuiwezesha serikali kuwa na mapato ya kutosha kugharamia mipango yake ya maendeleo ikiwemo michezo.

 

Tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre mjini kwa uratibu wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoa Kigoma likiwa na ujumbe wa shukrani kwa mlipa kodi.

 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kali alisema kuwa serikali itasimamia kwa karibu kukamata na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaoingiza bidhaa nchi kwa njia za magendo.

 

Kwa upande Naibu Kamishna Mkuu wa TRA,Mcha Hassan alisema kuwa  mikutano na mabonanza wanayofanya imekuwa na faida kubwa kutokana na kuongezeka maradufu kwa wigo wa walipa kodi lakini pia watu wengi wamekuwa wakipata elimu na hamasa ambayo imesaidia kukabili changamoto mbalimbali za kikodi kwenye biashara zao.

 

Katika bonanza hilo timu ya walipa kodi wafanyabiashara wa manispaa ya Kigoma Ujiji walifanikiwa kuwa mabingwa katika mpira wa miguu huku wafanyakazi wa TRA wakiibuka na ushindi wa kuvuta Kamba.

 

Michezo mbalimbali ilichezwa katika bonanza hilo ikiwemo kukimbia mbio fupi za mita 100 ambapo Abdul Mohamed aliibuka Mshindi kwa wanaume na Habiba Ziaidi mshindi wa wanawake , Festo Lukelo mshindi kukimbiza kuku huku Mussa Avia akiibuka mshindi kukimbia na magunia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI