Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Changamoto zinazowakumba watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi na magumu zimetakiwa kushughulikia kwa ukaribu na jamii inayowazunguka ili kupunguza wimbi la watoto hao ambao wanapoteza ndoto zao kwa kukosa msaada.
Vituo vya watoto yatima vimeanzishwa kwa ajili ya kusaidia katika malezi ya watoto hao ambao wamekosa msaada ambapo Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Njombe imezulu na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wa kituo cha Compasion Foundation COF kilichopo mjini Njombe ikiwa ni kilele cha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Njombe Specioza Owure amesema wamefika kutoa misaada katika kituo hicho kutokana na changamoto za kimalezi wanazopitia watoto hao na hivyo wameona umuhimu wa kuwafikia na kuwapa mahitaji yakiwemo magodoro,sabuni,mafuta pamoja na kiasi cha shilingi laki sita kwa ajili ya bima ya afya kwa baadhi ya watoto.
Nahoda P Nahoda ni Kaimu mkurugenzi msaidizi utawala ambaye amemwakilisha kamishna wa TRA nchini anasema watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wanapaswa kupatiwa msaada kwani ndio wanaoweza kuja kulisaidia taifa katika siku za usoni.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha watoto Yatima cha Compasion Foundation kilichopo Air port mjini Njombe Sister Lusia Mlowe amesema hivi sasa kituo hicho kina watoto 30 ambao wanachukuliwa kwenye mazingira magumu huku akiishukuru TRA kwa jitihada zake katika kuwasaidia.
Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya msingi COF Semen Msigwa amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuwashika mkono katika malezi ya watoto hao.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo hicho akiwemo Macrina Mahali na France Mgimba wamekiri kupokea misaada hiyo na kwamba itawasaidia katika maisha yao.
Kilele cha wiki ya shukrani kwa mlipa kodi kinahitimishwa kwa kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii pamoja na kutoa tuzo kwa walipa kodi wazuri ambao wamefanya vyema katika kulisaidia taifa kukusanya maduhuri ya serikali.
0 Comments