Mkuu wa Wilaya wa Masasi Lauteri John Kanoni , muwakilishi Mkuu wa Mkoa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Mtwara na kuwataka wahitimu kuhakiksiha kuwa wanazingatia misingi ya uaminifu na uadilifu katika jamii wanayoenda kuihufumia.
Akizungumza katika maafali ya kwanza katika tawi hilo huku yakiwa ya 21 kwa chuo hicho amesema kuwa anamatumaini makubwa na wahitimu hao ambapo anaamini kuwa watakuwa mabalozi wazuri katika kukitangaza chuo hicho na watazingatia ujuzi waliopata ndani ya chuo hicho na kutumia maarifa hayo.
Mkuu huyo amewasihi wahitimu hao kundelea kuelimishashana na kujitengenezea fursa za kibiashara huku wakitambua mchango wa chuo hicho ambao ni mkubwa wa kutoa fani mbalimbali wenye weredi kwenye fani za uhasibu, ununuzi, ugavi, usimamizi wa biashara na rasilimali.
“Ongezeni juhudi ya kutoa elimu iliyobora inayowajenga wahitimu na kuwapa uwezo wa kuajiri na kuajiriwa bila kusahau ubunifu wao ambao utawasadia kushiriki katika fursa zitakakazo jitokeza za kujenga muhimili ya taifa kiuchumi na kwa teknologia ya kisasa” amesema Kanoni
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TIA, Wakili Said Musendo amesema kuwa katika kipindi cha miaka sita chuo hicho kimewezesha baadhi ya kampas kuweza kujenga majengo yao ya kudumu hivyo kuwepo hapa kwetu ni faraja na mafanikio makubwa.
“Ni vema mkajua kuwa leo wahitimu mnapa karatasi moja tu ya ukubwa wa A4 mtakuwa wanatalaamu na mabalozi wa tia sio wote mtakao kuwa waajiriwa serikali tumieni ujuzi mliopata ili kuwaboreshea uchumi wenu ili kuwapa nafsi watanzania kunufaika na limu wanayopata” amesema Musendo
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa William Pallangyo amesema kuwa wanazo kampas saba za Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Kigoma na Singida ambapo kwa mtwara pekee kuna wahitimu 436.
"Tumefanya maafali leo katika kampasi yetu ya mtwara ambapo yameenda sambamba na kutambulisha kampasi hiyo yameenda sambamba na kutambulisha uanzishwaji wa Shahada ya kwanza katika Kozi za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi na Uongozi wa Rasilimali Watu kozi hizi zitatolewa chuoni hapo" amesema
0 Comments