Header Ads Widget

SHILINGI BILIONI 67 KUWEZESHA WANAFUNZI WASICHANA KUPATA ELIMU YA UJUZI

 

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo

Viongozi wa serikali na wadau wa maendeleo wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mradi WEZESHA BINTI unaotekelezwa na Shirika la ENABEL

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Zaidi ya Shilingi Bilioni 67 Sawa na UERO milioni 25  zinatarajia kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuwezesha wasichana wadogo kupata elimu bora itakayowezesha wasichana hao kupata elimu bora na ujuzi mambo yatakavyqawezesha kupata  kazi za staha baada ya masomo yao.

 

Hayo yameelezwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la maendeleo la serikali ya Ubelgiji nchini Tanzania (ENABEL), Koenrad Goekint wakati wa uzinduzi wa mradi wa miaka mitano unaojulikana kwa jina la WEZESHA BINTI ambao utatumika kuinua uwezo wa wasichana na walemavu kielimu na kuweza uwiano Sawa kwenye suala la jinsia.

Koenraad alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo jumla ya shule 25 katika mkoa Kigoma zitafikiwa ambapo wanafunzi wasichana na wanafunzi wavulana walemavu 12,750 watafikiwa.

 

Alisema kuwa katika shule hizo 25 shule nane zitajengewa mabweni yatakayokuwa na kila kitu kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi hao ikiwemo mfumo wa teknolojia ya Computer,shule kuwekewa  mfumo wa vyoo vya kisasa vyenye mfumo wa maji safi na maji taka huku walimu 500 wa sekondari wakipatiwa mafunzo kwa ajili ya kuwezesha kufundisha masomo ya hisabati na sayansi.

 

Akizungumza wakati akizindua mradi huo Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema mradi huo ni muhimu kwa mkoa Kigoma katika kuinua hali za wasichana kielimu lakini kuwasaidia kuingia kwenye soko la ajira wakiwa na ujuzi ambao hautawafanya kuwa watu wa kuomba kusaidiwa.

 

Kutokana na hilo ametaka viongozi na watendaji wa mamlaka mbalimbali za serikali,taasisi zisizo za serikali na wananchi kwa jumla kuunga mkono mradi huo na kutoa nafasi kwa wanafunzi wanaolengwa kufanikisha yale yanayokusudiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI