Mtendaji mkuu wa Taasisi ya uhasibu Tanzania(TIA)Profesa William Pallangyo akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 21 TIA na ya kwanza kwa kampasi ya Kigoma yaliyofanyika katika viwa ja vya mwanga centre
Na Editha Karlo,Kigoma
WAHITIMU wa Taasisi ya uhasibu(TIA)kampasi ya Kigoma wametakiwa kusimamia vyema fedha za umma pindi watakapopata ajira katika taasisi mbalimbali ili elimu na mafunzo waliyopata chuo hapo yaweza kuwa na Tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 21 ya TIA na ya kwanza kwa kampasi ya Kigoma yaliyofanyika katika viwanja vya Mwanga centre Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalii kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye aliwataka wahitimu kuwa washauri wazuri na wanaofuata sheria na taratibu katika kazi zao.
“Usimamizi wa fedha za umma una changamoto,ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG)imekuwa ikieleza juu ya ubadhirifu wa fedha za umma hata kwenye miradi ambayo serikali inatekeleza niwaombe wahitimu mkipata nafasi za kujiriwa au kujiajiri mkawe washauri wazuri”alisema
“Nimepita kwenye mabanda nimeona umahiri wenu na kutupa wasaa wa kushuhudia matunda na juhudi zenu hivyo kwa niaba ya serikali nitoe pongezi kwa uongozi wa Taasisi,wahadhiri na wafanyakazi wote kwa kazi nzuri katika kipindi chote mlichokuwa kwenye mafunzo yenu chuoni”alisema
Alisema Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt Samia Suhulu Hassan imekuwa mstari wa mbele katika katika kuunga mkono juhudi za kuboresha elimu kwa nyanja mbalimbali.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Wizara TIA wakili msomi Said Musendo aliwataka pia wahitimu kuwa wazalendo na kuhakikisha wanaenda kutatua changamoto katika jamii kupitia taaluma zao,pia aliwataka wahitimu kujiendeleza zaidi kielimu ili kuweza kumudu soko la ushindani la ajira.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya uhasibu(TIA)Profesa William Pallangyo alisema jumla ya wanafunzi 910 wamehitimu fani mbalimbali katika kampasi ya Kigoma,ambapo kwa mwaka 2022/23 wahitimu 13,218 kutoka kampasi za Mbeya,Singida,Mwanza,dar es Salaam na Kigoma wamehitimu fani mbalimbali.
Katika mahafali hayo mtendaji mkuu wa Taasisi alitambulisha masomo mapya ngazi ya shahasa katika uhasibu,ugavi na manunuzi,usimamizi wa biashara na uongozi wa rasilimali watu ambapo masomo hayo yatakuwa yanatolewa kampasi ya Kigoma.
Alisema pia chuo kinaendelea na ujenzi wa madarasa yake katika eneo la Kamala ili waweze kutoka kwenye majengo ya kupanga wanayotumia sasa,ujenzi huo unafadhiliwa na serikali ya awamu ya sita ambapo hadi kumalizika utagharimu shilingi bilioni 11,kwasasa ujenzi umefikia asilimia 25.
“Mradi huu wa chuo katika eneo la Kamala ni fursa kwa wakazi wanaoishi jiranu na chuo kwani wataweza kupata ajira ambazo ni rasmi na zisizo rasmi hivo kufanya hali ya kipato chao kuongezeka.
Baadhi ya wahitimu katika fani ya manunuzi na ugavi wamesema pia safari yao ya masomo haikuwa rahisi ilihitaji uvumilivu,ushirikiano,nidhamu,kujituma na zaidi kumtegemea Mungu sababu yeye ndiyo amewezesha wao kufika hapo
Wahitimu hao wamehaidi kwenda kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata sheria na miongozo waliyofundishwa ili kupunguza dosari mbalimbali zilipokatika taaluma yao.
Mwisho
0 Comments