NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amewataka viongozi wa Wilaya ya Nyamagana, kwimba, Ukerewe, Sengerema na Ilemela kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo ifikapo mwanzoni mwa muhula mpya wa masomo 2024.
Ameyabainisha Hayo katika Kikao kazi Cha wadau wa elimu chenye lengo la kujadili mikakati ya kupokea watoto watakaojiunga na shule awali, Msingi na sekondari Mkoani humo.
Makalla amesema kuwa Halmashauri zote zinapaswa kukamilisha miundombinu ya madarasa kama serikali inavyoagiza ili kutoa nafasi Kwa watoto waliofikia umri wa kujiunga na shule na wanaoanza ili waweze kuanza masomo yao, kamati za Usalama na watendaji kushirikiana Kwa pamoja kukomesha utoro.
"sitarajii kusikia mtumishi au kiongozi anakula sikukuu sehemu fulani ndani ya huu muda wakati mpo Asilimia 45 ya utekelezaji wa agizo la kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu, fanyeni kazi usiku na mchana " Alisema Makalla.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Martine Nkwabi amesema kuwa jumla ya shule za Msingi 991 za Mkoa huo zilifanya mtuhani wa kumaliza elimu ya Msingi 2023 Kwa watahiniwa 92, 655 ambapo watahiniwa 78,437 ikiwa ni Asilimia 84.7 huku wavulana wakiwa wamefaulu 36.397 na wasichana wakiwa 42.040.
0 Comments