NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MWANZA.
Mwanaume mmoja ajulikane Kwa jina la Nestory John mwenye miaka 52 mkulima na Mkazi wa Buhongwa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza ameakatwa na jeshi la polisi Kwa tuhuma za kuhusika na kuchoma moto nyumba na kusababisha vifo vya watu watatu.
Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani humo Wilbord Mtafungwa amesema kuwabmtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 07.12.2023 majira ya saa 00:20 usiku eneo la Lwanhima katika Wilaya hiyo kuchoma nyumba ya Eva Stephano ilichomwa moto na kusababisha vifo hivyo na uhalifu wa Mali.

"Upelelezi na msako mkali ulifanyika na jeshi letu nankubahatika kumkamata mtuhumiwa aliyetenda kosa kinyume na sheria za Nchi" Alisema Mtafungwa.
Hata hivyo ameeleza kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi utakamilika kutokana na kutenda kosa kinyume na sheria
0 Comments