Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Halmashauri ya mji wa Njombe imehakikishia wazazi na walezi kuwa miundombinu yote ya elimu imeboreshwa tayari kwa kuwapokea wanafunzi wa darasa la Kwanza na Kidato cha kwanza hapo januari 2024 na hivyo kusiwepo kwa kisingizio kitakachosababisha watoto wasiripoti shule.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mwaka mpya ujao na kwamba vikwazo vya kimiundombinu katika sekta ya elimu vimeondoshwa na hivyo watoto wanatakiwa kupelekwa shule pindi muhula mpya wa masomo utakapoanza.
Aidha Mpete amesema serikali imepeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo ukiwemo ya elimu na hivyo zinapaswa kuunguzwa mkono kwa kusomesha watoto katika mazingira rafiki na yanayofikika.
Sanjari na hayo lakini pia amesema halmashauri hiyo imepokea kiasi cha shilingi milioni 583 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Kata ya Makowo kutokana na kukosa shule na kusababisha wanafunzi kutembea umbali mrefu.
0 Comments