Na Shemsa Mussa,Kagera
Akieleza changamoto ya Maji ilivyo katika kijiji cha Buchurago katika kata ya Bugorora ndani ya Wilaya ya Missenyi Meneja Ruwasa wilayani humo Eng Endrew Kilembe amesema changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji katika kijiji hicho ilipelekea wananchi kuanza kutumia maji ambayo sio safi na salama .
Amesema kwa mazingira hayo wameweza kupeleka Mitambo kwa ajili ya kuchimba visima virefu vitakavyowezesha kusambaza maji ndani ya kijiji kizima na wananchi wataondokana na changamoto hiyo iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.
"Tunategemea ndani ya week mbili yaani siku 14 tutakuwa tumemaliza kuchimba kisima tunafanya haraka kama dharura kwa sababu ya changamoto iliyotokea hivi karibuni katika kijiji hiki ya ugonjwa wa Mlipuko kwahiyo tutatumia jitihada zote ili tupate maji safi kwa haraka ili tuone kama tutapunguza na kuzuia kuenea kwa ugonjwa hu.amesema Eng kilembe"
Aidha Eng kilembe ameongeza kuwa Wilaya ya Missenyi ina jumla ya kata 20 na mpaka sasa zimekamilika jumla ya Asilimia 78 ya upatikanaji wa Maji katika kata zote na amesema kuwa wamejitahidi kupeleka Huduma ya Maji katika maeneo mengi na maeneo yaliyobaki ni machache.
Amesema katika wilaya ya missenyi kuna miradi ya maji inayoendelea na katika mwaka 2023-2024 zimetengwa kiasi cha Shilingi Bilion 4.9 kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali ya Maji na utekerezaji umeshaanza ambapo upo mradi katika kijiji cha Ngando na mradi huo unahudumia vijiji vitatu Ikiwemo Ngando,Byeju na Nkerenge.
Pia amesema upo mradi wa maji ambao tayari umeanza kutumika na wananchi wameanza kupata huduma ya maji uliyopo katika kata ya Nshunju mradi huo unahudumia kata nzima yenye vijiji viwili vya Nshunju na Kiilima na mradi huo umeghalimu kiasi cha Shilingi Bilion 1.1
"Nafikiri mwaka ujao wa fedha tutafika mpaka asilimia 85 kwa sababu lengo la serikali ni kufika asilimia 85 ifikapo mwaka 2025 na sisi watu wa Ruwasa Missenyi tunajitahidi sana naamini tutafika asilimia hiyo.amesema Eng Kilembe
"
Hata hivyo Eng Kilembe amewasisitiza na kuwataka wananchi kutunza na kulinda vyanzo vya maji hasa panapojenjwa miradi ya maji kutokukata mabomba ,na kusema kuwa miundo mbinu yote ya maji ni kwa ajili ya wananchi na ni mali yao huku akisema yakikatwa mabomba inaweza kutokea ukosefu wa maji kwa muda mrefu na kuipatia hasara kubwa serikali inayotekeleza mahitaji hayo kwa wananchi na watanzania kwa ujumla .
Ikumbukwa kuwa hivi karibuni ililipotiwa taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu katika kijiji cha Buchurago kata ya Bugorora wilaya ya Misenyi mkoani Kagera idadi ya wagonjwa 18,huku 6 wakiendelea na matibabu katika zahanati ya Buchurago na wagonjwa 8 tayari wameruhusiwa kutoka hospital baada ya afya zao kuhimalika na jumla ya watu wa 4 wakipoteza maisha
Kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo watalamu wa afya wameendelea na jitihada za kutoa elimu na vifaa kinga kwa wananchi ili kuhakikisha ugonjwa huo hauendelee kusambaa zaidi.
0 Comments