Header Ads Widget

MONGELLA- SIMAMIENI MIUNDOMBINU YA SHULE PAMOJA NA VIFAA VYOTE

 


Pamela Mollel ,Arusha 


Walimu wote Mkoa wa Arusha wametakiwa kusimamia utunzaji wa miundombinu inayojengwa pamoja na vifaa vyote vinavyowekezwa kwenye shule zao.


Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John  V.K Mongella wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya shule, ikiwa ni maandalizi ya mapokezi wanafunzi, muhula wa masomo unaotarajia kuanza, Januari 2024


 Pia Mongella ameonyeshwa  kukerwa kwa baadhi ya majengo na vifaa kuanza kuharibika kutokana na uangalizi mbovu.


Mhe. Mongella amewaagiza walimu wote, kusimamia utunzaji wa majengo na vifaa vyote vya shule, ikiwa ni pamoja na kutumia asilimilia 35 ya fungu la ukarabati kupitia fedha za uendeshaji wa shule, kufanya matengenezo madogo madogo pindi unapotokea uharibifu.


" Serikali inatumia fedha nyingi kuyajenga majengo haya  kuweni wazalendo,  simamieni na wajengeeni uwezo wanafunzi kuthamini na kutunza vifaa vya shule" alisema Mongella.


Aidha, amewasisitiza kutambua  nia ya Serikali ya kuwekeza fedha nyingi, ni kuhakikisha mazingira ya kujifunza na kufundisha kwa  walimu na wanafunzi, yanakuwa bora na rafiki, hivyo walimu na wanafunzi wanalo jukumu la kutunza vifaa vyote vya shule



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI