Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wananchi wa Kata ya Uru Kusini kama katika harambee ya kujenga nyumba ya Mapadri katika kigango cha Chombo.
Katika harambee hiyo, viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Uru Kusini Fredrick Mbararia, pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wa Kanisa.
Wakisoma risala, Mbunge alielezwa kuwa ujenzi wa nyumba hiyo ya Mapadri utagharimu shilingi milioni 400, na hadi sasa zimetumika shilingi milioni 170 ambapo Waumini wa Kigango cha Chombo wanajitahidi ujenzi ukamilike ili Mapadri na watumishi wengine wa Kanisa wahamie mapema iwezekanavyo.
Akiongoza harambee hiyo, Mbunge aliwatia moyo Waumini kwa kuwakumbusha kuwa kutoa ni moyo na sii utajiri na kuwaambia kwamba ni wajibu wa kila mkristu kulijenga kanisa pamoja na kuwakumbusha kuwa wakimtolea Mungu ni kwamba yeye atawainua.
Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,013,800 ilipatikana kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa nyumba hiyo.
Mwisho.
0 Comments