Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROFESA PATRICK NDAKIDEMI ASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIUATILIFU VYA MAZAO MJINI MOSHI

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 

MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameshiriki katika uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza viuatilifu vya mazao kiitwacho Plant Biodefenders Limited kilichopo Shirimatunda, Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro ambacho kina uwezo wa kutengeneza wastani wa lita 2,000 kwa siku.



Kiwanda hicho kilizunduliwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa David Silinde kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe.



Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda hicho, Silinde alimpongeza mwanzilishi wa kiwanda hicho kwani kitasaidia sana kutatua matatizo yanayowakabili wakulima wa Tanzania.


Alisema, Wizara ya Kilimo itaziweka bidhaa za kiwanda hicho katika programu ya Serikali ya ruzuku za kilimo.



Alipopewa fursa ya kutoa salamu, Prof Ndakidemi alimpongeza sana mwanzilishi wa kiwanda hicho Dr Never Mwambela Zekeya ambaye alimsimamia katika masomo yake ya shahada ya uzamivu (PhD). 


Alisema, msomi huyo amefanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuanzisha kiwanda kitakacho saidia taifa kutoka kwenye PhD yake na kutoa wito kwa vijana wasomi kutoka vyuo vikuu vya Tanzania kuiga mfano wa Dr Zekeya.



Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro,  Wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Mkuu wa Chuo Cha Wanyamapori Mweka,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa na Wilaya, Madiwani kutoka Manispaa na Halmashauri za Moshi, viongozi wa dini na wadau wa maendeleo wa mashirika ya kimataifa.

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI