Na Shemsa Mussa,Kagera
Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi wilaya ya Karagwe chini ya Mwenyekiti wa chama hicho wilaya Paschal Rwamugata imeiagiza mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Bukoba (BUWASA) kusimamia vizuri mradi wa maji wa Nyakasimbi uliopo Wilayani humo ili ukamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Karagwe Paschal Rwamugata alitoa agizo hilo wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya wilaya ilipofanya ukaguzi wa maendelea ya ujenzi wa mradi wa maji wa Nyakasimbi unaotekelezwa chini ya Buwasa.
Rwamugata alisema kuwa kamati ya siasa baada ya kuona upungufu uliopo katika mradi huo uliofikia asilimia 65 mpaka sasa atahakikisha anafanya kila liwezekanalo ili iletwe kwa ajili kukamilisha mradi huo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyakasimbi Valence Kasumuni alisema kuwa Wananchi wa maeneo ya Nyakasimbi wanakabiliwa na changamoto ya maji kwa kuyafuata umbali mrefu kwa muda mrefu hivyo kukamilika kwa mradi huo itakuwa neema kwa Wananchi hao.
Kwa upande wake katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe Rasuli Shandala kwa niaba ya mkuu wa wilaya Karagwe ameziomba kamati za siasa ngazi ya kata kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao na kuisemea kwa Wananchi.
Wakati huo huo Chama Cha mapinduzi Ccm Wilayani humo kupitia kamati ya siasa imekagua mradi wa maji wa Ihembe one unaogharimu zaidi ya shilingi Bilioni Moja na kuagiza shirika la umeme Tanzania Tanesco kuhakikisha linarahisisha huduma ya umeme katika chanzo hicho.
Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi Ccm Paschal Rwamugata aliyeambana na wajumbe wa kamati hiyo katika ziara ya kukagua miradi inayosimamiwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini -Ruwasa.
Rwamugata alisema tayari serikali inaendelea kutekeleza maazimio yake kama ilivyo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020/2025 ya kumtua Mama ndoo kichwani upande wa maji hivyo changamoto ya umeme wa Tanesco katika chanzo hicho isikwamishe jitihada.
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini Ruwasa mhandisi Cassian Wittike alisema mradi huo mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 95 na unaendelea kuwahudumia wananchi wapatao 3,498 wa Ihembe one kwani ili kuruhusu huduma kuendelea iliwalazimu kufunga umeme wa jua(Sola) kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi huku wakisubiri pia umeme wa Tanesco kwani wamekwisha kupeleka maombi.
0 Comments