Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati kilele cha wiki ya shukrani kwa mlipakodi kikifikia tamati nchini Tanzania,Kampuni ya ununuzi na uuzaji parachichi mkoani Njombe ya Avo Africa imepokea tuzo ya mshindi wa jumla ya mlipa kodi bora kutokana na ufanisi mkuwa wa kufanya biashara kwa kuzingatia sheria za nchi.
Awali meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Njombe Specioza Owure amesema katika kipindi cha mwezi Julai wakati wa kuanza mwaka mpya wa fedha wa 2023/2024 wamefikia ufanisi wa zaidi ya asilimia 100 katika makusanyo.
Kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Nahoda Nahoda katika hafla ya utoaji tuzo hizo amesema mchango mkubwa ambao unatolewa na walipa kodi ndio unaofanikisha TRA kufikia malengo ya makusanyo.
Kampuni ya ununuzi Parachichi mkoani Njombe ya Avo Africa chini ya mkurugenzi wake Nagib Karmal imesema imefanikiwa kupata tuzo hiyo kutokana na kufanyakazi hiyo kwa kuzingatia sheria za nchi hususani katika kipengere cha ulipaji kodi.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe Siphael Msigala amewafahamisha wafanyabiashara kusini mwa Tanzania kuwa tayari serikali imeanzisha chombo kitakachosikiliza changamoto za wafanyabiashara pasina kuvuka mipaka.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe ameipongeza TRA kwa kuvuka lengo katika makusanyo yake huku akielekeza weledi kuzingatiwa katika kazi.
Katika tuzo hizo Uplands fm Radio pia imepokea tuzo ya mlipa kodi na mhamasishaji bora wa kodi mkoani Njombe
0 Comments