Askari Wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe wamefariki dunia baada ya kupata ajali iliyohusisha gari ndogo aina Toyota SIENTA iliyokuwa imebeba askari hao waliokuwa katika majukumu yao ya kikazi na Lori lililokuwa Iikitokea jijini Dar Es salama Kuelekea nchini Zambia .
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahmud Banga amesema askari waliokufa kwenye ajali hiyo ni WP .7866 Coplo Elizabeti kizale (36) na H.1027 Coplo Patrick Salehe huku chanzo cha ajali kikielezwa kuwa ni uzembe uliofanywa na dereva wa gari ndogo ambaye aliingia barabarani pasipo kuchukua tahadhari.
Ameongeza dereva wa Lori hilo alikimbia na kuacha gari mara tu baada ya ajali hiyo na miili ya askari hao imehifadhiwa hospitali wakati taratibu za kuisafirisha zikifanyika.
0 Comments