Header Ads Widget

ANDENGEYE ATAKA MAONO YA NYERERE YAISHI MIOYONI MWA WATANZANIA

 


Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye akipanda mche wa zao la chikichi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara ambapo kimkoa ilifanyika kata ya Machinjioni Manispaa ya Kigoma Ujiji 

(Picha na Fadhili Abdallah)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amewaongoza viongozi na wananchi wa mkoa huo kupanda miche ya michikichi katika mitaa mbalimbali ya manispaa ya Kigoma ikiwa ni kupamba sherehe za miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara huku akitaka viongozi na wananchi kuishi na agizo la Marehemu Mwalim ulius Kambarage Nyerere kupiga vita maadui watatu wa Taifa.

Katika maadhimisho hayo ambayo kimkoa yalifanyika kwenye kata ya Machinjioni Manispaa ya Kigoma Ujiji Andengenye aliongoza upandaji wa miche zaidi ya Miche  2000 ya michikichi na kusema kuwa miche hiyo iwe ishara ya kudumisha amani na mshikamano wa Watanzania.

Akizungumza na wakazi wa kata ya Machinjioni Manispaa ya Kigoma Ujiji kabla ya kugawa miche hiyo na kuongoza zoezi la upandaji miche hiyo ya michikichi  Mkuu huyo wa Mkoa wa Kigoma alisemakuwa  ni jukumu la kila mwananchi kukabiliana na maadui watatu wa Taifa ambao ni ujinga, maradhi  na umasikini agizo lililotolewa na Marehemu Baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere lakini linaishi mpaka sasa.


Mkuu huyo wa mkoa alisema  kuwa jamii itafaulu kukabiliana na maadui hao watatu iwapo  kila mtu atatekeleza majukumu yake kwa ufasaha, kujituma katika uzalishaji mali pamoja na kudumisha amani na utulivu hali itakayosababisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kuimarika na kulifanya Taifa liweze kusonga mbele.

katika kutekeleza kazi mbalimbali zinazokwenda sambamba na maadhimisho hayo, mkuu huyo wa mkoa ameshiriki kufanya zoezi la usafi katika Soko la wakulima la Nazareti lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli amesisitiza jamii wilayani humo kujenga tabia ya kudumisha usafi ili kukabiliana na athari mbalimbali zinazoweza kusababishwa na maradhi yatokanayo na uchafu na kupunguza nguvu kazi ya Taifa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI