Na Fadhili Abdallah, Kigoma
Wananchi wa mji wa Uvinza mkoani Kigoma wametakiwa kulinda maeneo yao badala ya kuyauza sasa kwani ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) utayafanya maeneo hayo kuwa na thamani kubwa baada ya mradi huo kuanza kazi.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alisema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye mji mdogo wa Uvinza akiwa kwenye mfululizo wa mikutano ya hadhara kwenye majimbo manane ya mkoa Kigoma.
Zitto alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo Uvinza patakuwa njia panda ya kipande cha reli hiyo kwenda Msongati na Gitega nchini Burundi na mizigo itakuwa ikishushwa happ hivyo kutafanya eneo hilo kuwa eneo la kibiashara jambo ambalo linaifanya ardhi ya eneo hilo kuongezeka thamani, Pamoja na hilo Zitto ameitaka halmashauri ya wilaya Uvinza kulipima eneo la wilaya hiyo la mji mdogo wa Uvinza, kuipanga na kuliweka kwenye mpango kabambe ili kuendana na kasi ya mabadiliko.
Awali Waziri Kivuli wa mifugo na Uvuvi wa ACT Wazalendo, Kiza Mayeye alisema kuwa bado migogoro ya ardhi eneo la Uvinza imekuwa kikwazo kwa wananchi kutumia maeneo yao kwa shughuli za uchumi, Kutokana na hilo Mayeye alisema kuwa ni vizuri serikali ikaimaliza migogoro hiyo na kuwafanya wananchi hao kufaidi eneo lao kuwa kituo cha biashara kunakotokana na ujenzi wa reli hiyo ya kisasa na barabara za kiwango cha lami inayotekelezwa.
Mwisho,
0 Comments