Header Ads Widget

WAZIRI NDALICHAKO:WAAJIRI WATOE KIPAUMBELE CHA AJIRA KWA WENYE ULEMAVU TANZANIA.

 

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Ajira,Kazi,Vijana na wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAAP NJOMBE

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu Kazi,vijana,Ajira na wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amesema serikali imeanza kununua vifaa mbalimbali vya kuwasaidia watu wenye ulemavu wakiwemo wasioona huku waajiri wakisisitizwa kutoa kipaumbele cha ajira  kwa wenye ulemavu kwa asilimia 3 kwa mujibu wa sheria.


Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo wakati wa kilele Cha maadhimisho ya  siku ya wasioona Fimbo nyeupe yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe ambapo amesema serikali itaendelea kuwashika mkono walemavu wote na ndio maana imekuwa na utaratibu wa kutoa mikopo ya asilimia 2 kwao kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri pamoja na mahitaji mengine.

Aidha Amesema kiasi cha shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya kukarabati vyuo vya watu wenye ulemavu huku kiasi cha shilingi bilioni 4.5 zimenunua vifaa vya watu wenye ulemavu ikiwemo miwani ya macho,Fimbo Nyeupe na Vishikwambi.


Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema jitihada kubwa zimefanyika na serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha hata watoto wenye ulemavu wanapata haki ya kupata elimu hivyo jamii isiwafiche watoto ndani.

Mwenyekiti wa chama Cha wasioona Tanzania TLB Omary Mpondelwa na Subira Shedangio Kaimu katibu mkuu Taifa chama hicho wameiomba serikali


Kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu kwani hakuna aliyependa Wala anayetamani kuwa mlemavu licha ya jitihada kubwa zinafanyika.


Kwa upande wao watu wasioona akiwemo Pascal Msigwa mwenyekiti wa TLB Mkoa wa Njombe na Nuru Awadh mkurugenzi wa taasisi ya wanawake na wasichana wasioona Tanzania wamesema wangali wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutengwa na kutotazamwa kwa karibu kama watu wengine.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Fimbo Nyeupe kwa mwaka huu inasema''Upatikanaji wa teknolojia Fikivu Katika ujenzi wa uchumi wa kidigitali ni mkombozi kwa mtu asiyeona na Taifa''.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI