Header Ads Widget

WAZIRI MKUU MAJALIWA AVUTIWA NA CHUO KIKUU CHA IRINGA

 


WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Kassim Majaliwa amepongeza jitihada Kubwa zinazofanywa na chuo kikuu cha Iringa  katika utoaji elimu inamwezesha mhitimu kujiajili katika Sekta binafsi .

Huku akiwataka wahitimu Vyuo vikuu kuwekeza katika ubunifu zaidi ili Watu wengine kufika chuo kikuu cha Iringa kujifunza .

Akizungumza leo wakati wa Mahafali ya chuo hicho alisema katika ya vitu ambavyo Serikali inajivunia na kupongeza chuo hicho ni jinsi inavyowaandaa Vijana kuja kuwa wajasiliamali wazuri.

Alisema Serikali imekuwa shahidi wa ubora wa elimu inayotolewa katika chuo hicho kwani wapo Viongozi waziri kama Stevin Lyabato ,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albart Chalamila ,DC Kebani Kihongosi na wapo majaji ambao wamehitimu katika chuo hicho akiwemo Mbunge wa Iringa Mjini Jesca Msambatavangu na MNEC Richard Kasesela .


"serikali inajivunia chuo hicho cha Iringa kwa ubora wa elimu na Mimi naendelea kuwatia Moyo wote wanaosoma kwenye chuo hiki kikuu maarufu chuo kikuu cha Iringa"

Alisema kuwa kwa wale wanaoendelea kusoma na wale wanaohitaji kujiunga na chuo hicho waendelee kujivunia chuo kikuu cha Iringa .

Majaliwa ambae alimwakilisha Rais Dr Samia Suluhu Hassan katika Mahafali hiyo alisema Serikali ya awamu ya sita inajivunia chuo hicho na Vyuo vingine nchini kwa kuendelea kutoa elimu bora.

Alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia inaendelea kuboresha mfumo Bora wa elimu kwa ajili ya kuona elimu inayotolewa inakuwa Bora zaidi .

Hata hivyo alisema Serikali ipo kwenye maandalizi ya kujenga  Vyuo vikuu 14 nchini katika mikoa ya pembezoni Ili kuongeza wigo ya elimu zaidi .

Alisema kuhusu ombi la mabweni katika chuo kikuu cha Iringa analichukua na kulipeleka kwa Mheshimiwa Rais Dr Samia.

"Na Mimi namuunga Mkono mheshimiwa Rais kwa jibu atakalotoa kwa ajili ya kusaidia Ujenzi wa mabweni kwa kuchangia Shilingi milioni 10"

Alisema Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu Ili kuwezesha wanafunzi wenye vigezo Kupewa fedha hizo za mikopo . 

Alisema ili kuongeza wigo wa mikopo ya elimu ya juu Serikali ya awamu ya sita imeelekeza kuongeza fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi Ili kuongeza udahili wa wanafunzi nchini .

Hata hivyo alisema Serikali inajivunia kuona jitihada Kubwa zinazofanywa na Vyuo vya taasisi za dini na Vyuo binafsi katika kuendelea kutoa elimu mbali mbali zikiwemo elimu za ufundi .

Alisema kuwa akiwa katika mabanda ya maonesho ndani ya chuo kikuu cha Iringa ameshuhudia Vijana wabunifu wa kada mbali mbali .

Hivyo kuagiza Halmashauri nchini kuendelea kutenga fedha za makusanya ya ndani Ili kutoa mikopo nafuu kwa makundi mbali mbali .

Huku aliwataka wahitimu kutumia Mafunzo na elimu waliyopata chuoni hapo kwenda kuonesha tofauti ya wao wasomi na wale ambao hawajabahatika kufika chuo kwa wao kutumia elimu hiyo kubuni shughuli za uzalishaji Mali .

Pia kutokana na Kasi ya mabadiliko ya teknolojia ni lazima kwenda kuendena na mabadiliko hayo kwa ajili ya kulitumikia Taifa ikiwa ni pamoja na kwenda kuchangamkia mradi wa Jenga kesho iliyo bora  mradi ambao Serikali imewekeza fedha nyingi.

Kuhusu Ukatili wa Kijinsia alisema ni lazima taasisi zote za elimu ya juu nchini kuhakikisha zinatekeleza maelekezo ya serikali ya kuanzisha madawati ya kupinga Ukatili wa Kijinsia katika Vyuo .




















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI