Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la uwekezaji litakalofanyika Novemba 16 kutangaza fursa za kiuchumi jijini Tanga
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ametangaza Kongamano la kiuchumi linalolenga kuimarisha uchumi wa mkoa huo baada ya Serikali kuwekeza katika sekta mbali mbali ikiwemo Bandari na Bomba la mafuta
Alisema kuwa Mkoa wa Tanga utafaidi sana na Kongamano hilo likifungua fursa za uwekezaji na kuonesha maendeleo yaliyofanyika haswa katika upanuzi wa Bandari ya Tanga na ujenzi wa Bomba la mafuta
"Awali Bandari ya Tanga imeboreshwa na kuimarishwa Serikali ya awamu ya sita mama yetu ameupiga mwingi kwa kumimina bilion 429.1 na kuifanya Bandari ya Tanga kuwa moja ya Bandari yenye ubora kina kimeongezwa na upana umeongezwa Meli kubwa sasa zimeanza kushuka Tanga"alifafanua Kindamba .
Kongamano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga litahudhuriwa na Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi na Mabalozi wa nchi mbalimbali wanaowakisha hapa nchini huku wengine wakiwakilisha kwa njia ya mtandao.
0 Comments