NA AMINA SAIDI, TANGA
Waandishi wa Habari wameaswa kuandika habari zenye kuleta matokeo chanya kwa jamii zitakazoweza kuchochea mabadiliko juu ya kuondokana na ukandamizaji na unyanyasaji wa kijinsia.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa umoja wa vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya usawa wa kijinsia kwa wanachama 27 wa klabu za mikoa ya Tanzania bara na Visiwani.
Mkurugenzi Kenneth amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuondoa changamoto ya ukandamizaji na unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika ili kufikia malengo ya Serikali katika kukabiliana na tatizo hilo.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka waandishi hao kutumia fursa ya mafunzo hayo kwa kuandaa vipindi na kuandika habari ambazo zitakazoleta mabadiliko.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika Mkoani Morogoro yameandaliwa na umoja wa vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC).
0 Comments